HOTUBA
YA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA BANK OF AFRICA - TANZANIA BALOZI
MWANAIDI SINARE MAAJAR WAKATI WA UZINDUZI WA TAWI JIPYA LA BANK OF AFRICA
ZANZIBAR, TAREHE 3 MACHI 2016
Mheshimiwa Mgeni rasmi, Waziri wa fedha wa
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, Ndugu Omar Yussuf Mzee,
Mkurugenzi mtendaji wa BANK OF AFRICA - TANZANIA,
Ndugu Ammish Owusu- Amoah,
Wakurugenzi wa Bodi,
Wapendwa wateja,
Wafanyakazi wa BANK OF AFRICA - TANZANIA,
Ndugu Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana,
Ninayo furaha kubwa
kuwakaribisha nyote katika tukio hili
muhimu la kihistoria kwa BANK OF AFRICA -
TANZANIA.
Namshukuru Mwenyezi Mungu
mwingi wa Rehema kwa
kutuwezesha sote kuwa hapa leo, na pia shukrani zangu za
dhati
kabisa ziende kwa mgeni wetu rasmi, Mheshimiwa Omar Yussuf
Mzee - Waziri
wa Fedha wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwa kuchukua muda adhimu nje ya
ratiba yake yenye
mambo mengi muhimu ya kitaifa na kuweza kujumuika nasi katika
kuadhimisha uzinduzi huu wa Tawi letu jipa la BANK
OF AFRICA hapa Zanzibar.
Napenda pia
kuwakaribisha wakurugenzi wetu wa bodi ya BANK
OF AFRICA, wateja wetu wapendwa
na sote tuliojumuika hapa
jioni hii ya leo kushuhudia BANK OF AFRICA – TANZANIA
ikipiga hatua nyingine katika kukuza mtandao wa benki yetu
Tanzania.
Mabibi na Mabwana
BANK OF AFRICA -
TANZANIA ni benki ya kibiashara
ilioanzishwa Juni 2007 hii ni baada ya kuinunua
Eurafrican Bank
iliokuwepo Tanzania tangu Septemba 1995 ikiwa na matawi
matatu.
BANK OF AFRICA ipo katika nchi 18 za Africa na yenye
makao makuu yake Dakar,
Senegal. Kwa hapa nchini Tanzania
BANK OF AFRICA ina makao makuu yake jijini
Dar es Salaam
tayari ikiwa na matawi 22
pamoja na kituo kimoja cha biashara
pale
Dar es Salaam kwajili ya kuhudumia wateja wakubwa.
Katika miaka 9, BANK
OF AFRICA - TANZANIA imeonyesha
maendeleo mazuri na hata kujichukulia nafasi nzuri
miongoni mwa
benki muhimu katika sekta ya kibenki nchini Tanzania. Benki
imeleta mchango endelevu kwa watanzania. Hili linaonyeshwa na
uwezo wa benki
kupeleka matawi yake katika maeneo mbalimbali
ya Tanzania ikiwemo: Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Moshi,
Mwanza,
Mbeya, Tunduma, Morogoro, Kahama, Mtibwa na
Mtwara. Katika miaka hii tisa pia
benki imeweza kutengeneza
faida zaidi ya billioni 7 za kitanzania.
Katika kutambua
mahitaji ya wateja BANK OF AFRICA inakuja
na huduma stahiki ambazo zitaweza
kumfikia kila mzanzibari kwa
urahisi zaidi hii ni katika kutimiza ari ya benki
isemayo “focused
on development in the heart of Africa” yaani: kulenga
maendeleo
katika moyo wa Africa. Bodi ya wakurugenzi pamoja na uongozi
wa BANK
OF AFRICA umeendelea bila kuchoka kuweka nguvu
katika maendeleo ya kila
mtanzania hii ikionyeshwa na uamuzi wa
benki kufungua tawi hili la 22 la BANK
OF AFRICA ZANZIBAR.
Mabibi na Mabwana
Takwimu zinaonyesha Zanzibar
imeendelea kujenga uchumi imara
na endelevu, ufanisi katika mfumo wa fedha ni
moja ya mahitaji ya
muhimu na ya msingi katika ukuaji wa uchumi na maendeleo
kwa
ujumla. Tukiwa na hili akilini BANK OF AFRICA iliona
umuhimu wa kuwekeza
hapa Zanzibar ili kuendeleza ukuaji wa uchumi. BANK OF AFRICA – TANZANIA
imetengeneza huduma katika muundo bora ambao ni rahisi kutumia na utakao mfaa
kila moja watu kwa mahitaji yake hii ni katika kurahishisha utunzaji wa fedha,
utoaji wa mikopo na hata uwekezaji.
Zanzibar inafahamika
kwa uwezo wake mkubwa katika kilimo
hasa cha karafuu, uvuvi, biashara na
utalii. Thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma Ilikuwa milioni 229 Dola za
kimarekani ikilinganishwa na milioni 203 Dola za kimarekani katika mwaka
unaoishia Januari 2014. Thamani ya bidhaa zinazouzwa nje imeongezeka kwa asilimia
23, kwa kiasi kikubwa ukuaji huu wa uchumi umechangiwa hasa na biashara ya viungo,
Karafuu ikiendelea kutawala soko la nje na kufikia asilimia 51.8 kuishia
Januari mwaka 2015.
Katika kufungua tawi hili
jipya hapa Zanzibar BANK OF
AFRICA- TANZANIA imekuja na huduma
zilizotengenezwa rasmi kufikia na kutimiza mahitaji ya wateja wetu. BANK OF
AFRICA - TANZANIA pia tupo katika mchakato wa kuangalia jinsi ya kutoa huduma
ya “Islamic Banking” ili kuhudumia na kufikia mahitaji ya wateja wetu.
Mabibi na Mabwana
BANK OF AFRICA -
TANZANIA tupo hapa ili kuleta mageuzi
katika sekta ya kibenki tukiweka nguvu
zetu zote katika ukuaji wa
uchumi wa Zanzibar na ukuaji wa sekta ya kifedha.
Tupo tayari
kufanya kazi nzuri na wananchi wa Zanzibar na ninaimani kwamba uwepo wetu utaleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa Zanzibar.
Napenda pia
kuipongeza menejimenti na wafanyakazi wa BANK
OF AFRICA - TANZANIA, kwa kujitoa
kwao na kufanya kazi
kwa bidii katika kufanikisha hili tunaloshuhudia leo. Bila
Juhudi
zao tukio hili lisinge kuwa na mafanikio haya makubwa
tunayoyashuhudia.
Kwa maneno haya
machache, kwa mara nyingine tena, nichukue
nafasi hii kumshukuru Waziri wa
Fedha wa serikali ya mapinduzi
ya Zanzibar kwa kukubali kujumuika nasi leo na
pia napenda
kuwakaribisha nyote katika uzinduzi rasmi wa tawi letu jipya hapa
Zanzibar.
Asante.
No comments:
Post a Comment