Habari za Punde

JKU Waelekea Ruvu Kujiandaa na Mchezo Wao na SC Villa ya Uganda.

Klabu ya maafande wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar, JKU wameelekea mkoani Ruvu Tanzania bara kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wao wa kimataifa barani Afrika.


Akizungumza na Blog hii meneja wa kikosi hicho Meja afande Chimudi alisema kikosi tayari kimeshatua mkoani humo kwa ajili ya kambi hiyo.


Chimudi alisema wachezaji wote walisajiliwa na JKU wapo kwenye kambi hiyo ambayo itaenda sambamba na safari yao ya kuelekea nchini Uganda kuikabili Sports Club Villa wiki ya pili ya mwezi huu.


"Tumeamua kubadilisha upepo kutoka Dar es salaam hadi huku Ruvu naanimi kwa hali ya hewa ya Uganda na huku haitokuwa na mabadiliko sana".Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Malale Hamsini Keya kinaiwakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya kombe la Shirikisho barani Afrika na kimefanikiwa kuingia hatua ya pili baada ya kupata ushindi wa mezani kufuatia wapinzani wao Gaborone United ya Botswana kujitoa kwenye ngarambe hizo.Baada ya kumaliziaka kwa michezo ya wiki iliyopita JKU itachuana na klabu hiyo ya Uganda kuanzia tarehe 11-13 ya mwezi huu wakianzia ugenini yaani nchini Uganda.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.