Habari za Punde

Kwa hili mlilowafanyia wanawake ZLSC hongera lakini………

Na Haji Nassor, Pemba
Wakati tukiwa katika wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, wanawake wa Zanzibar tuseme si haba zipo taasisi zimekuwa mstari wa mbele katika kuwapa wanawake elimu ya sheria na elimu ya uraia.
Kwa miaka kadhaa wanawake wengi hasa walioko vijijini, walikosa uwelewa katika nyanja hizo, hali iliopekelea wale wenye nia na madhumuni ya kuwakandamiza kupata nafasi pana.
Wiki hii ya kuelekea Machi 8, ambayo ndio kilele cha siku yenyewe, wanawake wa Mikoa miwili ya Pemba, walishapata uwelewa wa haki za binadamu, na elimu ya uraia mafunzo yaliondaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba.
Sasa hapa lazima, kama ZLSC ililfanya hilo wanawake wenyewe wawe makini na mstari wa mbele, kuwafahamisha wenzao, maana inawezekana ZLSC haina uwezo wa kuwaita wanawake wote wa Pemba.
Kwa hili nasema hongera Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, lakini wanawake waliopewa mafunzo hayo kamwe wasiyakalie na kuwakosesha wenzao.

ZLSC, ilisaka wafadhili kila kona ya ulimwengu, ili ipate nyenzo za kifedha kwa lengo la kuandaa mafunzo maalumu ya haki za binadamu na elimu ya uraia kwa wanawake wa wilaya zote nne za Pemba, sasa lazima waliopata wayasmbaaze.
Kama tuna kumbu kumbu, basi wapo idadi kubwa ya wanawake wamekuwa wakivunjiwa haki zao za binadamu na kukaa kimnya, inawezekana kwa kutoajua, sasa mafunzo hayo yawe mwanga.
Lakini pia usishangae kuwa wapo wanaume wamekuwa wakiwadhulumu au kuwanyima haki wanawake kama vile za mirathi, umiliki wa mali ma kusoma, akijua kwamba mwanamke huyo hana uwelewa, lakini sasa hayo yaondoke.
Mimi naamini kwa wanawakle 80 wa Pemba waliopewa mafunzo hayo na ZLSC na kama kila mwanamke mmoja kupitia vikundi vyao ya ushirika ataamua kutoa elimu hiyo kwa wanawake 10 basi wanawake 800 watakuwa na uwelewa wa haki za binadmu na elimu ya uraia.
Mini ninachoamini wanawake wanapendana sana ila tamaduni za wakoloni,ndizo zilizowagawa na ndio maana sasa imekuwa rahisi kwa kundi la wanaume kuweza kuwagawa.
Lakini tukielekewa Machi 8, hebu basi wanawake hasa hawa waliopewa mafunzo na ZLSC muukate mzizi huu kwamba hampendani, na anzeni kuwaelimisha wenzenu haki zao.
Si mnavyovikundi vyenu ambavyo vimekusanya wanachama wengi wakiwa wanawake, basi kuelekea maadhimisho hayo, sio vibaya hata kidogo mkajiweka kwenye maeneo mkaelimishana.
Iweje kwamba wanawake 80 wapewe mafunzo tena yanayohusu haki na wajibu wa wanawake, kisha wengine waendelea kukosa elimu hiyo wakati mmoja aliepo katika eneo alishirikia mafunzo hayo ya siku mbili.
Ndio maana hata Mratibu wa ZLSC Fatma Khamis Hemed, wakati akiyanfunga mafunzo hayo, yeye alisisitiza zaidi suala la mafunzo waliopatiwa wanawake kupeana, maana kwa muda mrefu waliishi kwenye wingu la kutengwa.
Kama hayo hatoshi, hata Afisa mdhamini mwenye dhamana ya wanawake na watoto Pemba, Maua Makame Rajab yeye alikwenda mbali zaidi, kwamba mafunzo hayo yatakuwa na tija pindi wakiwaelimisha wenzao.
Yoye kwa yote, hongera Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na hasa tawi la Pemba, kwa kuwakusanya wanawake pekee na kuwafahamisha haki, wajibu wao kwenye taifa lao.
Lakini nanyi wanawake mliopewa mafunzo hayo, basi onyesheni ari ya kupendana kwa kuwapa wenzenu waliomo ndani ya vikundi na hata nje, maana ukimuelimisha mwanamke ndio jamii hiyoo.
ZLSC mafunzo kwa wanawake hayo yasiwe ya mwanzo na mwisho, bali wanahitaji zaidi, maana historia inatuonyesha kundi hilo lilitelekezwa tokea enzi za ukoloni, hadi leo hawajaachiwa kwa asilimia mia moja.
Naamini kila kitu kinawezekana, iwapo kila mmoja atafanya wajibu na jukumu lake bila ya kusimamiwa na rushwa kwake ikawa ni mwiko.

Mwandishi anapatikana kwa hajinassor1978@gmail.com.    

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.