Dk. Mehul A. Shah, Mtaalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka
Hospitali za Apollo; Hyderabad
Na Mwandishi wetu,
Siku ya Figo duniani, ni tukio la
kimaarifa na la kuleta mwangaza duniani linaloadhimishwa mwezi Machi. Kila
mwaka, kumekuwepo na shughuli mbalimbali kitaifa na kimataifa zinazofanywa na
mashirika mbalimbali ya Figo, mahospitali, wataalamu wa afya na watu binafsi
wanaotaka kuleta mabadiliko duniani dhidi ya ugonjwa wa figo. Ni muhimu
kuhimiza elimu, vipimo vya awali, na mtindo mzuri wa maisha ili kuruhusu Jamii
itambue magonjwa ya Figo yanayoathiri watu milioni duniani ikiwemo watoto ambao
wapo katika hatari ya kuugua katika umri mdogo. Kampeni ya mwaka 2016 ina lengo
mahususi kwa magonjwa ya Figo na watoto.
Matatizo ya figo kwa watoto yajulikanayo
kitaalamu kama (Paediatric Nephology aliments) yanahusiana na magonjwa ya Figo
kwa watoto wachanga na watoto wadogo mpaka miaka kumi na nane. Kwa mujibu wa Dk. Mehul A. Shah, Mtaalamu wa magonjwa ya
figo kwa watoto kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad Magonjwa ya Figo kwa
watoto yanaweza tokea Sababu ya mapungufu katika ukuaji au maumbile
(yanayotokea wakati wa kujifungua), kurithi (katika familia) au mabadiliko
katika mazingira/ kinga mwilini au madawa. Matatizo Kama hayo yakitambulika
mapema huweza zuia uharibifu wa Figo.
Dk.
Shah anawahimiza watanzania kufwata mbinu za kuzuia matatizo ya Figo
kwa watoto ambazo zitasaidia kujenga Tanzania isio na magonjwa ya Figo. Mbinu
izi ni kama Kupima mkojo kwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka miwili wenye
homa kali, kuhimiza watoto wasiozidi miaka mitatu kukojo kwa wakati (wasibane
mkojo), ulaji wa matunda na mbogamboga, chumvi ya kiasi na nyama katika milo ya
familia.
Kupunguza muda unaotumika na watoto
katika televesheni na kompyuta na kuongeza shughuli nyingi Zaidi zenye
kupunguza ongezeko la uzito, kuepuka dawa za kupunguza maumivu kama Nimesulide,
Ibuprofen n.k. pamoja na madawa ya Ayurvedic/Unani, matumizi ya Crocin/ Calpol/
Paracetamol, kupima presha angalau mara moja kwa mwaka kwa watoto wenye Zaidi
ya miaka mitatu, kufanya uchunguzi wa ugonjwa
wa Figo kwa mtoto mwenye matatizo katika ukuaji, anemia, shinikizo la damu, damu
katika mkojo, kuvimba kwa mwili au maambukizi ya mkojo ya mara kwa mara. Mbinu
hizi pia zimetajwa na Dk. Shah kama
njia za kuepuka magonjwa ya Figo kwa Watoto.
Matatizo ya Figo yanaweza tokea kwa
watoto kutokana na matatizo katika maumbile au yanayotokea baada ya kuzaliwa.
Wataalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka Hospitali za Apollo wanahimiza upimaji wa mara
kwa mara ili kufahamu kama mtoto wako ana matatizo ya figo.
No comments:
Post a Comment