Habari za Punde

Taarifa kwa Umma;Kufutwa kwa Safari za Ndege APRILI 2, 2016



Tunaomba radhi sana kwa taarifa kwamba  idadi kadhaa ya abiria wetu walishindwa kufika kwenye maeneo  waliyokusudia  jioni ya Aprili 2, 2016.

Hii ilitokana na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa taa kwenye njia ya  kurukia  kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro na hivyo kukosekana kwa usalama  ambao ungewawezesha marubani wetu  kutua.

Huu ni mfululizo wa matukio ambayo yalisababisha  kufutwa kwa ndege mbili miongoni mwa ndege zetu kutua  usiku ule:

  • Ndege Na. FN157 iliondoka kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa  3.18 usiku ikitarajiwa kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro kabla ya muda  unaotakiwa  saa 4.40 usiku. Wakati ndegte ikikaribia  Uwanja wa Kilimanjaro marubani wetu walijulishwa  na mnara wa kuongozea ndege  kwamba taa zilizopo kwenye njia ya kurukia ndege  zilikuwa hazifanyi kazi lakini hali ingetengemaa  muda usiokuwa mrefu. Ndege ilizunguka  uwanja wa Kilimanjaro  ikisubiri  ukarabati wa taa hizo kwa  takribani  dakika 30 kabla ya kurudi Dar es salaam kwa kuwa taa hizo zilikuwa bado hazifanyi kazi.
  • Ndege iliwasili tena Dar es Salaam saa 5.20 usiku na abiria walibaki kwenye  ukumbi wa kusubiria ndege  wakati ndege  ikijazwa mafuta tena na marubani wakiandaa mpango mpya wa kusafiri tayari  kurudi Kilimanjaro mapema kadri  iwezekanavyo pindi ukarabati wa taa kwenye njia ya kurukia ndege  ukikamilika. Kwa bahati mbaya taa hizo zilikuwa hazifanyi kazi  hadi kufikia saa  saa 7.00 usiku wa kuamkia Aprili 3, 2016,  ambapo muda sahihi na salama kwa marubani wa  ndege ukiwa umemalizika kwa kuwa walishakuwa  kazini kuanzia saa 12.30 jioni.
  • Hii inamaanisha kwamba  hatukuwa na mbadala wa kufuta  safari, na hivyo ndege Na. FN158 ambayo ilikuwa  irudi  kutoka Kilimanjaro kuja Dar es Salaam.
  • Abiria wetu waliopata usumbufu walipewa nafasi kwenye ndege iliyokuwa inafuatia  na ilisafiri kutoka uwanja wa pili  kurudi kule walikotoka. Baadhi ya abira  walichukua mbadala huu lakini wengie waliamua kubaki  katika uwanja wa ndege  kusubiri ndege  iliyofuata.
  • Abiria wote  walioomba kupatiwa usafiri kwenye ndege iliyofuata walisafiri nasi kwa  kuelekea maeneo waliyokuwa wanakwenda Aprili 3, 2016.

  • Tunaomba radhi kwa abiria  wetu waliokuwa kwenye safari ile kwa usumbufu  walioupata huku tukiwahakikishia kuwa tunaweka kipaumbele kikubwa  kwenye usalama wa abiria wetu na marubani.

John Corse,
Meneja Mkuu, fastjet Tanzania

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.