Habari za Punde

Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS)

Katibu wa Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Bi. Moza Rajab Baraka , akitowa maelezo kabla kwa kuaza kwa Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo Maeneo Huru ya Uchumi Amani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Ndg Khatib Mwadini Khatib akitowa maelezo kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali kuizindua Bodi hiyo.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali akihutubiwa wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi hizo Maeneo Huru ya Uchumi Amani Viwanda Vidogovidogo Zanzibar kulia Mwenyekiti wa Bodi hiyi Profesa Ali Seif Mshimba na kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya Viwango Zanzibar (ZBS) nDG Khatib Mwadin Khatib.
Wazizi wa Viwanda Biashara na Masoko Mhe Balozi Amina Saluzindua Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar, (ZBS)
Wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar wakifuatilia Uzinduzi huo wa Bodi yao na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali.
Wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibara wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakifuatilia uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Zanzibar, baada ya uteuzi wa Bodi hiyo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Bodi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Profesa Ali Seif Mshimba akizungumza na kutowa shukrani kwa Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Balozi Amina Salum Ali, na kuwatambulisha Wajumbe wa Bodi hiyo wakati wa Uzinduzi wake uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Amani Viwanda Vidogovidogo Zanzibar.
Wafanyakizi wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) wakifuatilia uzinduzi huo wa Bodi yao  uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo Amani Viwanda Vidogovidogo Zanzibar.
Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali akiwa na Uongozi wa Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Ali Seif Mshimba na kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Ndg Khatib Mwadin Khatib, waliosimama nyumba ni Wajumbe wa Bodi hiyo kutoka kushoto Dk Burhan Othman Simai, Ndg. Makame Mbaraka, Bi Hamisa Mmanga na Ndg Saleh Suleiman Hamad. wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Uzinduzi huo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.