Habari za Punde

Polisi wategua mchezo mchafu wa kikosi kazi za kudhibiti magendo


Na mwandishi wetu, Pemba
KARAFUU kavu vipolo saba, ambavyo ni miongoni mwa vipolo 28 vilivyokamatwa na askari wa doria inayoendeshwa na vikosi vya SMZ, zikiwa zinataka kusafirishwa magendo, na kisha kutangaaza vipolo 21, hatimae Jeshi la Polisi wilaya ya Wete Pemba, limefanikiwa kuvifichua vipolo hivyo saba.
Taarifa za uhakika ilizozifikia Gazeti hili, zinaeleza kuwa kikosi hciho kilichowekwa kwa ajili ya kudbiti magendo, kilifanikiwa kukamata vipolo na gunia 28, ingawa kwenye vyombo vya habari walitangaaza vipolo 18 na magunia matatu ya karafuu yaliochanganywa na makonyo.
Baada taarifa hizo kutolewa kwa vyombo vya habari, siku ya pili yake taarifa zikaeleza kuwa, Polisi wilaya ya Wete walilifanya upekuzi kwenye nyumba za wananchi wawili shehia ya Ukunjwi na kufanikiwa kupata vopolo sita na nusu, ambavyo vinadaiwa ni sehemu ya zile zilizokamatwa na kikosi kazi.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa, ingawa mkuu wa familia ya nyumba hiyo Salmin Soud hakuwepo majira hayo wakati Polisi wakiongozwa na sheha wa shehia hiyo wakifanya upekuzi, lakini hatimae walifanikiwa kuondoka na mzigo huo.
Jeshi la Polisi lilifanikiwa kupata taarifa hizo kutoka kwa raia wema, kwamba nyumba mwa Salmin anaeishi shehia ya Ukunjwi Jimbo la Gando, kuna karafuu zimewakwa na kikosi kazi cha kuzuia magendo, na hatimae Polisi kuzifanyia kazi taarifa hizo.
“Mimi niliposikia taarifa hizi kwenye mtaa wangu, niliwapigia simu Polisi Wete, na baadae mchan walikuja na kufanya upekuzi chini ya sheha wetu, na walikamata karafuu hizo’’,alifafanu mwananchi ambae alikataa kutajwa jina lake lichapishwe.
Aidha mwananchi mwengine, alisema yeye aliona watu wakiwa wamejitiwisha mapolo hakujuwa mna kitu gani wakiziingiza ndani ya nyumba, ingawa aliskia harufu ya karafuu, na kutoa taarifa kwa wenzake na kisha jeshi Polisi kufika.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa, mara baada ya kikosi hicho kazi cha kuzuia magendo kufanikiwa kuzikamata guni na vipolo 21 ambavyo baadhi vilikuwa vimetiwa makonyo, na kuzipakia kwenye boti yao aina ya ‘fiber, walisita eneo la Ukunjwi na kupunguza mzigo huo.
Sheha wa shehia ya Ukunjwi Mkongwe Kasanja Khamis alipoulizwa juu ya tukio hilo ndani ya sheha yake, alikiri kuwapokea Polisi hao kutoa kituo cha Polisi Wete na kufanya upekuzi kwa ruhusa yake.
Alieleza kuwa, juzi majira ya saa 5:40 na saa 6:00 mchana walifikwa na Polisi kutoka Wete na kumuomba awapeleke safari yao na kutii agizo hilo, na walipofika kwa wananchi wawili akiwemo Salmin Soud walifanya upekuzi.
“Mimi nilichokishuhudia ni upekuzi kwenye nyumba mbili za wananchi wangu, na kisha kuwaona Polisi wakiondoka na mapolo mengi yakiwa na harufu ya karafuu, lakini kilichoendelea sikijui tena’’,alifafanua sheha huyo.
Akizungumza kwa njia ya simu mmoja wa maofisa wa KMKM Pemba, ambae hakupatikana jina lake, alisema yeye sio msemaji wa kikosi hicho, na kumtaka mwandishi yeyote anaetaka taarifa hizo na nyengine kwenda Unguja makao makuu kwa mkuu wa KMKM.
“Sikiliza mwandisi nenda Unguja Makao makuu yetu huko ndio utapa taarifa zote za Pemba na nyengine, lakini mimi sina mamlaka ya kutoa taarifa zozote”,alisema na kukata simu.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba Issa Juma Suleiman, alipouliza juu ya kadhia hiyo, alikana kukamatwa kwa karafuu hizo polo saba na anachofahamu yeye ni karafuu vipolo 18 na gunia tatu zilizokamatwa na kikosi cha kuzuia magendo.
“Wewe kama unataka taarifa za kukamatwa karafuu, wasiliana na KMKM ndio waliopewa kazi hizo na ndio waliokamata, sisi hatujakamata karafuu popote”,alifafanua Kaimu Kamanda huyo.
Juzi kikosi hicho kazi cha kuzuia magendo, kilitangaaza kukamata vipolo 18 vyenye karafuu kavu na magunia matatu makonyo, yamekamatwa zikiwa tayari kusafirishwa magendo wilaya ya Micheweni, ambapo mkuu wa operesheni hiyo Luteni Kanali Jabir Hamza, alisema karafuu hizo zimekamatwa Shehia ya Tondooni Wilaya ya Micheweni wakati wakiwa katika doria za kawaida.
Luteni Jabir alieleza kuwa Septemba 3, mwaka huu majira ya 10:00 alfajiri katika ufukwe wa bandari ya Tondooni wilayani humo, askari hao walizikamata karafuu pamoja na makonyo hayo zikiwa zinasubiri maji ya yajae ili ziweze kusafirishwa.
Hadi sasa kumeibuka utata mkubwa wa idadi ya karafuu kavu zilizokamatwa na kutangaazwa na kikosi hicho, ambapo inasemekana mmiliki wa mali hiyo ndie alietoa taarifa za idadi pungufu ya zilizokamatwa na kutaangazwa.

Tukio kama hilo liliibuka baina ya mwaka 2005 na mwaka 2007 eneo la Mkoani, ambapo KMKM walikamata idadi ya gunia zaidi ya 100 na kutangaaza gunia 60, ambapo baadae waliokuwa na mali hiyo walijitokeza na kuishitaki KMKM mahakama ya mkoa Chakechake

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.