Habari za Punde

Taasisi za Mikopo Ziwatazame na Wajasiriamali Wadogowadogo

Na Salmin Juma Pemba
TAASISI zinazotoa huduma ya mikopo zimetakiwa kuelekeza nguvu zake kwa kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo hasa wa maeneo ya vijijini kwa kuwapa mikopo yenye masharti nafuu na ambayo haina riba .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi , mjasiriamali Dadi Hamad Dadi mkaazi wa Madenjani Wilaya ya Wete kisiwani hapa ,ambaye anajishuhulisha na ukaushaji wa maembe alisema kwamba mikopo hiyo itamuwezesha kukuza mtaji pamoja na kuboresha bidhaa anayozalisha.

Alisema kwamba pamoja na ubunifu alionao , lakini bado taasisi zinazotoa mikopo zimeshindwa kutambua mchango wake katika kukuza pato la Taifa na kuzalisha ajira kwa vijana kwani lengo lake ni kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira .

Alieleza licha ya bidhaa anazozalisha kuwa na soko na uhakikisha nchi jirani ya Kenya , lakini ameshindwa kulitosheleza soko hilo kutokana na kutumia vifaa duni na ambavyo vinashusha ubora wa bidhaa hiyo .

Alifahamisha kwamba soko la bidhaa hiyo linatokana na ubora wa embe za Pemba , na kuongeza kuwa mbali na changamoto ya mtaji mdogo pia anakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya kisasa vya kukaushia embe .

Aidha alizidi kueleza kuwa kwa sasa anatumia sinia kukausha embe kutokana na kutokuwa na kifaa cha kisasa cha kukaushia embe pamoja na mashine ya kusagia viungo ambaavyo vinatumika kuchanganya ili kuifanya embe isiharibike.

“Ni vyema taasisi zinazotoa mikopo kuelekeza nguvu zake katika kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo hususani wa vijijini kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu na isiyo na riba jambo ambalo litapelekea kukua mitaji na kuimarika kwa kazi zaao za uzalishaji ”alieleza Dadi.

Diwani wa wadi ya Kiungoni Mussa Hossein Ayoub aliahidi kuwasilisha ombi maalumu katika Kikao cha baraza la Madiwani la kuitaka serikali kupitia Baraza la Mji kuunga mkono harakati za mjasiriamali huyo kwa kuhakikisha Baraza linashiriki katika kumtafutia vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi zake .

Alisema , wao kama w asimamizi wa serikali za mitaa wanapaswa kuunga mkono juhudi za wajasiriamali wadogo wadogo ambao wameonyesha nia ya kupambana na hali ya umaskini na hivyo kusaidia mikakati ya Taifa ya kukuza uchumi wake .

“Katika kikao cha baraza la madiwani nitapeleka ombi la kumsaidia kijana huyo ambaye ameonyesha nia ya kukabiliana na changamoto za maisha ili tutafute njia ya kumsaidia kufikia lengo alilolikusudia ”alieleza.

Hata hivyo , naye Mwenyekiti wa Baraza la Mji wa Wete Assa Juma Ali , mbali na kupongeza hatua aliyofikia kijana huyo kwa kubuni mradi huo , pia amemshauri kuzingatiwa suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira wakati anapotekeleza majukumu yake .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.