Habari za Punde

Wajasiriamali watakiwa kuboresha bidhaa ili kuleta ushindani

Na Mwandishi wetu, Pemba

Wajasiriamali kisiwani Pemba wameshauriwa kubuni  mbinu itakayoweza kuwasaidia kuboresha thamani ya bidhaa wanazozalisha na kuwaletea pato litakalowakwamua kiuchumi hapo baadae.

Wametakiwa kujikita katika kujifunza njia ya usindikizaji wa mazao na uwekaji wa vifungashio vinavyokubalika ili kuweza  kuleta  ushindani wa soko la bidhaa la  ndani na nje ya nchi .

Afisa uchumi kutoka idara ya uwezeshaji wizara ya wanawake na watoto Pemba Latifa Hassan Ali ameyasema hayo huko ukumbi wa uwanja wa Gombani Chake chake Pemba katika mafunzo ya usindikizaji wa matunda na mboga mboga kwa  wajasiriamali kisiwani Pemba.

Amesema changamoto inayowakabili wajasiriamali ni kukosa taaluma sahihi ya uzalishaji na mashirikiano ya pamoja kitu kinachochelewesha kupatikana kwa maendeleo endelevu miongoni mwao .

Nao baadhi ya wajasiri amali hao wameitaka serikali kupitia wizara ya uwezeshaji ,wazee , wanawake na watoto kuwatafutia mikopo ya  mashine za usindikizaji ili kuendana na  kasi ya maendeleo ya uzalishaji mali ulimwenguni ili bidhaa wanazozizalisha ziweze kupata soko kitaifa na kimataifa  .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.