Na
Abdi Shamnah
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema inasimamia na kuendeleza mageuzi ya Vyama vya
ushirika kwa kufuata taratibu, kanuni na sera, ili kuwa na vyama vyenye nguvu
na vyenye kuleta tija kwa wanachama.
Hatua
hiyo inakwenda sambamba na dhana ya umilikishaji wa vyama, ikiwa ni mwelekeo wa
kuviunganisha vyama vyote vidogo vidogo a vya kati, ili hatimae kuwa na SACCOS
kubwa ya Wilaya.
Hayo
yameleezwa kwa nyakati tofauti na Mkurugenzi wa Idara za vyama vya ushirika
Daud Simba, katika ufunguzi wa mikutano
mikuu ya ZASCCU kwa Mkoa ya Kusini na Kaskazini Unguja iliyofanyika Tunguu na
Kinduni.
Pamoja
na mambo mengine mikutano hiyo iliwachaguwa Weneyeviti, Makamo Wenyeviti na
wajumbe 10 (kila Mkoa) kwa lengo la
kuunda Bodi ya ZASCCU Taifa, ambapo itaishirkisha Mikoa mitano ya Unguja
na Pemba.
Akizungumza
na wanachama, Simba alisema kuna umuhimu wa viongozi watakaochaguliwa
kushirikiana na SACCOS zilizopo na kufanya akzi ya kuzinganisha ili kuwa na
SACCOS moja yenye nguvu, ili kufikia dhana ya kuweka akiba ya kutosha.
Alisema
viongozi wana jukumu la kuhamasisha uwekaji wa mitaji, na kufanya uwakilishi na
utetezi ili kuvijengea uwezo vyama hivyo.
Aidha
aliwataka wanachama hao kutokuwa na imani au huruma dhidi ya wale wote
wanaojinufaisha kupitia migongo ya wanachama na kutaka hatua za kisheria
zichukuliwe mara moja ili kujenga heshima ya vyama hivyo.
Mapema
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk.Muslih Hijja, aliwataka wanachama hao
kujiamini kwa kila wanachokifanya baada ya kufanya utafiti na kubaini faida na
hasara itakayopatikana.
Alisema
ili huduma za ufanisi ziweze kupatikana kupitia vyama hivyo, ni wajibu wao
kuzingatia suala la uaminifu, pamoja na
kushirikiana katika utendaji wa kazi.
Aidha
aliwataka kuwa wabunifu ili kuibuwa mbinu mpya pamoja na kujenga utamaduni wa
kujaribu, ili waweze kuongeza tija.
Nae
Katiobuy Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja,Mohammed Omar, kwa niaba ya Mkuu wa
mkoa huo kuzingatia umuhimu w akuwepo chombo hicho kwa lengo la kujenga nguvu
ya pamoja na kusukuma mbele malengo ya kuanzishwa kwa vyam vya akiba na kukopa.
Akizungumzia
uchaguzi huo, Omar aliwataka wanachama hao kuchaguwa mgombea kulinga na uwezo
alionao ili kufikia malengo ya kuwa na Bodi ya ZASCCU.
Alisema
serikali inashajiisha kuwepo kwa vyama imara ili kwenda smabamba na mpango wa
serikali wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini sambamba na kuibuwa ajira.
Katika
chaguzi hizo Ali Makame Juma kutoka North ‘B’ SACCOS, alichaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa ZASCCU Mkoa wa Kaskzini Unguja, wakati Abdulahalimu Ameir
akichaguliwa Makamo mwenyekiti.
Aidha
Juma Zungu Ameir alichaguliwa Mwenyekiti ZASCCU Kusini Unguja na Ameir Hashim
akiwa Makamo Mwenyekti.
No comments:
Post a Comment