Habari za Punde

Kitengo cha Maradhi Yasioambukiza (NCD)na Wizara ya Afya Zanzibar Waandaa Mdahalo wa Maradhi ya Kisukari katika Maadhimisho ya Maradhi ya Hayo Duniani.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Juma Malik Akili akifungua Mdahalo wa maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani uliowashirikisha wanafunzi kutoka Wilaya nane za Unguja katika Ukumbi wa Jengo la Utamaduni Rahaleo Mjini Zanzibar.
Mmoja wa washiriki wa mdahalo wa maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani kutoka Wilaya ya Mjini akitoa mchango wake kuunga mkono  mada inayosema ‘matumizi ya pombe na tumbaku yanapelekea kupata ugonjwa wa kisukari’.
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia mdahalo wa maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani  uliofanyika katika Ukumbi wa Jengo la Utamaduni Rahaleo  Mjini Zanzibar.
Viongozi wa meza  kuu wakifuatilia mdahalo wa maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani  uliofanyika katika Ukumbi wa Jengo la Utamaduni Rahaleo  Mjini Zanzibar. 

Jaji Mkuu wa mdahalo wa maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani uliowashirikisha wanafunzi kutoka Wilaya nane za Unguja Dkt. Faiza Kassim Suleiman akiwa na wasaidizi wake akitoa matokeo ya washindi wa mdahalo huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili akimkabidhi cheti cha mshindi wa kwanza mwakilishi wa skuli binafsi ya Trifonia Academy Nabil Mohd Mussa baada ya kuwa wapingaji wa mada inayosema ‘kisukari ni ugonjwa wa kitajiri’  katika mdahalo huo uliofanyika Ukumbi wa Jengo la Utamaduni Rahaleo Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.