Habari za Punde

KMKM chakamata mashua mbili zikiwa na mapipa 67 ya mafuta ya dizeli


Kikosi maalum cha kuzuia magendo KMKM kimekamata mashua mbili zikiwa na mapipa 67 ya mafuta ya disel katika maeneo ya bandari ya Fumba yaliyokuwa yanaingizwa Zanzibar kutoka Tanzania bara kinyume na sheria. 

Kepteni wa kikosi hicho, Khatib Khamis amesema mashua hizo zimkekamatwa majira ya saa 3 asubuhi jana katika doria zao za kawaida na wamiliki wa mashua wamekimbia. 

Nae afisa uhusiano wa Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB, Makame Khamis Mohamed amesema mafuta hayo watalazimika kuyapiga mnada na fedha itakayopatikanwa itaingia katika mfuko wa serikali kwa mujibu wa sheria. 

Hili ni tukio la tatu la kukamatwa vyombo vya baharini ndani ya mwezi huu katika ukanda wa bahari ya Zanzibar vikiwa na bidhaa mbalimbali zikiwemo mafuta na sukari zikisafirishwa kwa njia za udanganyifu kati ya Zanzibar na Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.