Habari za Punde

Lundo la Wachezaji Latua Azam Kwa Kujaribu Zari.


Uongozi wa Klabu Azam FC leo umefanikiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji kutoka Ghana, Enock Atta Agyei aliyekuwa akicheza timu ya Medeama.
 Agosti mwaka huu Azam iliingia makubaliano maalumu na Medeama juu ya kumsajili kinda huyo  anhezaji ayetimiza umri wa miaka 18 mwakani baada ya benchi la ufundi kuridhishwa na uwezo wake na sasa amejiunga rasmi kwenye viunga vya Azam Complex.

Agyei amesaini mkataba tayari  kuanza kuitumikia Azam katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara  mwakani pamoja na michuano mingine ikiwemo Kombe la Shirikisho Afrika.


Wana lambalamba hao wanaamini kuwa ujio wa nyota huyo wa timu ya Taifa ya Vijana ya Ghana chini ya miaka 17, utazidi kuipa nguvu timu yao kuelekea kwenye michuano mbali mbali itayokashiriki.
  
Wakati huo huo Wachezaji saba wamewasili leo kwa ajili ya kufanya majaribio ya kujiunga na vijana wa Kocha Zeben Hernandez ambao ni mabeki wa kati Mbimbe Aaron Nkot (Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast), kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Cameroon),

Wengine ni washambuliaji Yaya Awaba Joel (Cameroon), Samuel Afful, Benard Ofori (wote Ghana) na Konan Oussou kutoka Ivory Coast.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.