Na Salmin Juma, Pemba
Viongozi na wakuu wa utumishi wa umma nchini wametakiwa kuwa wakweli na wawazi na kufuata maadili ya utumishi ili kutekeleza wajibu wao kwa jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla ameyasema hayo katika ukumbi wa Makonyo Wawi alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya umuhimu wa maadili kwa wakuu wa Mikoa ,Wilaya na viongozi wengine wa umma Kisiwani Pemba .
Amesema kama viongozi wanapaswa hufahamu wajibu wao katika utendaji wa kazi wanazozifanya ili waweze kuaminika mbele ya jamii.
Naye Mwenyekiti wa Tume ya utumishi wa umma Zanzibar, Asaa Ali Rashid amesema lengo la mafunzo hayo ni kutekeleza matakwa ya sheria ya utumishi wa umma ya namba nne ya mwaka 2015 na kukuza uelewa wa maadili kwa viongozi hao
Amesema suala la maadili ni la kila mtu katika jamii hivyo viongozi ni lazima wawajibike ili kuondoa dosari miongoni mwa jamii.
No comments:
Post a Comment