Na Haji Nassor, Pemba
UONGOZI wa mahakama ya wilaya ya
Mkoani Pemba, umeiomba serikali kuangalia uwezekano wa kulihami haraka jengo la
mahakama hiyo, kutokana na kuvuja baadhi ya maeneo na kuwapa usumbufu wafanyakazi
wakati mvua inaponyesha.
Kauli
hiyo imetolewa na Kaimu, hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo Nassor Suleiman,
alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji, kwa Naibu waziri wa wizara nchi
afisi ya rais, Katiba, sheria utumishi wa umma na utawala bora, alipofika hapo
na jumbe wake, ikiwa ni sehemu za ziara yake ya siku mbili kisiwani Pemba.
Alisema
kuvuja kwa jengo hilo, wakati wakiwa kazini huwapa mashaka ya kuhama hama na
kusababisha kusita kwa kazi, kutokana na kukimbia maji kwa baadhi ya mapaa ya
mahakama hiyo.
Hakimu
huyo alisema, ingawa lipo paa walipata msaada wa kuezekewa na Baraza la mji
Mkoani, wakati wakifanya matengenezo ofisi yao, lakini kwa yaliobakia yapo
baadhi yanavunja na juhudi zinahitaji kuokolewa.
“Muheshimiwa
Naibu waziri tumeshaona juhudi za serikali za kulifanyia matengenezo makubwa
jengo letu la mahakama kuu Chakechake, lakini na hili la wilaya ya Mkoani, hali
iko mbaya maana yapo mapaa yanavuja’’,alifafanua.
Aidha
alisema changamoto nyengine inayowakumbuka wafanyakazai hao wa Idara ya
mahakama Mkoani, ni ukosefu wa usafiri kutokana na kuwa na vespa moja pekee.
Akielezea
changamoto nyengine inayowakabili, mfanyakazi wa mahakama hiyo Riziki Mohamed
Makame, alisema wanapata ugumu wa kusambaa baruza za wito ‘smears’ kwa
wahusika.
“Mahakama
inapotoa barua za wito, inatubidi tutumie nauli zetu, na kumuomba mtuhumiwa au
mlalamikaki ni kosa, sasa kama tukiwa na usafiri wetu, kazi itafanyika vyema.
Nae
mfanyakazi Muhidin Mohamed Muhidin, amelalamika kutoingizwa kwenye orodha ya
posho la shilingi 50,000 ingawa wenzao wa Unguja wameshaanza kupata.
Akilitolea
ufafanuzi hilo, Afisa Utumishi wa wizara hiyo Chumu Khamis Omar, alisema
lililojitokeza hadi wafanyakazi wa Pemba, kuchelewa kuingizwa kwenye posho
hilo, ni kuchelewa kupewa taarifa kutoka makao makuu Unguja.
“Ni
kweli wafanyakazi sasa kuna posho la mazingira magumo, kutoka shilingi 20,000
hadi shilingi 50,000, lakini kwa sisi wafanyakazi wa Pemba, tulichelewa maana
taarifa zilichelewa kutufikia’’,alifafanua.
Mapema
Naibu waziri wa nchi afisi ya rais Katiba, sheria Utumishi wa umma na utawala
Bora Zanzibar, Khamis Juma Maalim, aliwapongeza wafanyakazi hao licha ya
changamoto zinawazowakabili.
Kwa
upande wake Naibu Mrajisi wa Mahakamu kuu Zanzibra Ali Ameir, alisema kutokana
na changamoto zinazowakabili wafanayakazi hao, na kufanikiwa kufanya kazi, ile
dhana ya hapa kazi imewadia.
Ujumbe
huo wa Idara ya mahakama ikiambatana na Naibu waziri wa wizara hiyo,
wamekamilisha ziara ya siku mbili kisiwani Pemba, ambapo walitembelea jengo la
mahakama kuu Chakechake lililofanyiwa ukarabati, mahakama za Konde, Wete,
Kengeja na Mkoani.
Wakati
huo huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dk: Ali Mohamed
Shein, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa jengo la mahakama kuu
Chakechake lililofanyiwa matengenezo makubwa.
No comments:
Post a Comment