Habari za Punde

Jezi Mpya za Zanzibar Zaingia Mitandaoni

Chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar, ZFA kimepata mkataba wa jezi kwa ajili ya timu za taifa za visiwa hivyo.
                         JEZI YA UGENINI
Jezi hizo mpya zimetengenezwa na kampuni ya AMS Clothing ya nchini Australia na zitatumiwa na timu za taifa za Zanzibar katika michuano mbali mbali.
Mbali na Zanzibar, kampuni ya AMS Clothing ina mkataba wa kutengeneza jezi za timu za mataifa ya Rwanda, Sierra Leone na Sudani ya Kusini.
                        JEZI YA NYUMBANI
Mwakilishi wa AMS Clothing alisema wanatarajia kuuza jezi hizo katika mtandao huku lengo lao likiwa kuuza jezi hizo visiwani katika siku za usoni.
” Tulifanya kazi na Mzee Zam Ali wa ZFA kufanikisha kila kitu. Jezi ziliwasili Zanzibar wiki iliyopita. “

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.