Afisa
mfawidhi Kutoka tume ya haki za
binaadamu na utawala bora Pemba Bw Suleiman Salim Ahmad akitoa majibu ya
maswali mbalimbali yaliyoulizwa katika maadhimisho ya siku ya haki za binaabadamu
yaliyofanyika huko chakechake mkoa wa kusini Pemba chini ya kituo cha Huduma za
sheria afisi ya Pemba
Mratibu
wa kituo cha huduma za sheria afisi ya Pemba Bi Fatma Khamis Hemed akitolea
ufafanuzi michango na maswala mbalimbali yaliyoulizwa na washiriki katika
maadhimisho ya siku ya haki za binaadamu yaliyoandaliwa na kituo hicho
Meneja wa Zanzibar Saving and Credit
co-operative Union ( ZASCCU) Omar Abdalla Ali akiuliza swali katika
maadhimisho ya siku ya haki za binaadamu yaliyofanyika leo huko chakechake
Pemba na yaliyoandaliwa na ZLSC afisi ya Pemba ambapo alitaka ufafanuzi kwanini kituo kimejikita zaidi kwa akinamama
wakati haki ni kwa wote.
Mshiriki wa maadhimisho ya siku ya haki za binaadamu yaliyoandaliwa na
kituo cha huduma za sheria leo huko chakechake Muhammed Ali Muhammed akitaka
ufafanuzi juu ya kesi zinazopelekwa
mahakamani ambapo Jaji mkaazi hayupo, jee zinachukuliwa hatua gani
Ibrahim N. Kombo kutoka
JUMAZA akitaka kujua ni kwanini mahkama
inawanyima dhamana washtakiwa na pia kesi kuchukua muda mrefu bila ya kufikia tamati, ni katika maadhimisho
ya siku ya haki za binaadamu huko chakechake pemba, maadhimisho ambayo yameandaliwa na kituo cha
humuda za sheria afisi ya Pemba
Mshiriki katika
maadhimisho ya siku ya haki za binaadamu yaliyofanyika leo huko chakechake
Pemba yaliyoandaliwa na ZLSC afisi ya
Pemba bw: Yussuf Abdalla kutoka jumuiya ya maimamu Zanzibar akiuliza juu ya ucheleweshaji wa
upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto unasababishwa na nini.(Picha Salmin Juma - Pemba)
No comments:
Post a Comment