Habari za Punde

Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) Yafanya Usaili Kuwapata Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi Mdogo Jimbo la Dimani Zanzibar.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva (kushoto) akiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume na Sekretarieti cha Usaili wa kuwapata Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani, Zanzibar . Uchaguzi huo utakaofanyika Januari 22, 2017.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhan (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume wakati wa kikao cha Usaili wa nafasi ya Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Zanzibar. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damiani Lubuva na Kulia ni Mjumbe wa Tume Mhe. Mchanga Mjata.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.