Habari za Punde

Waziri wa Biashara Amani Salum Atembelea Kiwanda cha Coca cola.

Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali ameutaka uongozi wa CocaCola kufikiria kurejesha uzalishaji katika kiwanda cha Maruhubi na Serikali imeandaa mikakati ya kuvilinda viwanda vya Zanzibar ili wananchi wafaidike kupata ajira.
Amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni kuhakikisha bidhaa zote zinazoingizwa Zanzibar kutoka nje zinalipiwa ushuru unaostahiki na kudhibiti mbinu za wafanyabiashara za kukwepa kulipa kodi. 

Balozi Amina ameeleza hayo alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda CocaCola Maruhubi ambacho kinaendelea kusambaza soda zinazozalishwa Dar es salaam kufuatia kiwanda hicho kusitisha uzalishaji kwa muda mrefu sasa. 

Amesema kitendo cha kusitisha uzalishaji wa soda katika Kiwanda cha Maruhubi kinawanyima fursa wananchi wengi kutoa mchango wao na ni kinyume cha sera ya kuwa na viwanda venye tija. 

Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha CocaCola Zanzibar na Tanzania Bara Ndugu Haji Ali amemueleza Waziri Amina wamelazimika kusitisha uzalishaji Zanzibar kutokana na ushindani uliopo wa bidhaa hiyo kutoka nje bei yake kuwa chini kutokana na kuingizwa bila kulipiwa ushuru.

Ametaja sababu nyengine kuwa ni uchakavu wa mitambo ya uzalishaji iliyokuwa ikitumika imepitwa na wakati na haiendani na teknolojia ya usazalisha wa sasa.

Hata hivyo amesema Kiwanda cha CocaCola Zanzibar kimeongeza mauzo ya bidhaa za aina tofauti za soda zinazozalishwa Tanzania Bara kwa asilimia 40. imetolewa na Idara ya Habari maelezo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.