Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Jamuhuri Yaiwekea Gumu Timu ya Azam Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar Kulazimisha Sare ya Bila Kufungana.

Vikosi vua Timu ya Azam na Jamuhuri zikisubiri kukaguliwa na mgeni rasmin wa mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar. kabla ya kuaza kwa mchezo huo kwa timu hizo. Katika mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi kundi B uliokuwa na upinzani mkubwa kwa mashumbulizi ya kila upande hadi kipindi cha pili timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana. 
Kipindi cha pili cha mchezo huo kilikuwa na mashambuliza ya kupokezana. Timu ya Azam itabidi kujilaumu kutokana na washambuali wake kupoteza nafasi nyingi za wazi na kuokolea na Kipa wa Timu ya Jamuhuri kwa umahiri wake wa kuweza kuokoa michomo mengi golini kwake hadi mwisho wa mchezo huti timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.   
Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Abdallah Maulid Diwani akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Azam kabla ya kuaza kwa mchezo huo.
Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Abdallah Maulid Diwani akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Jamuhuri kabla ya kuaza kwa mchezo huo.
Wachezaji wa Timu ya Azam wakisalimiana na wachezaji wa Timu ya Jamuhuri kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar uliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar usiku, Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.katika dakika 90 za mchezo huo na kugawana poiti. 
Waamuzi wa Mchezo wa Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa mchezo huo.
Kikosi cha Timun ya Azam kilicholazimishwa sare ya 0-0 na Timu ya Jamuhuri kutoka Kisiwani Pemba katika michuano ya 11 ya Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar lililofanyika usiku katika uwanja wa amman.
Kikosi cha Timun ya Jamuhuri kilicho ilazimishwa Timu ya Azam katika michuano ya 11 ya Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar lililofanyika usiku katika uwanja wa aman.

Kizazaa golini kwa Timu ya Jamuhuri wakati wa mchezo wake wa Kombe la Mapinduzi na Timu ya Azam.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.