Habari za Punde

Mchezo wa Kombe la Mapinduzi Kati ya Yanga na Jamuhuri Uliofanyika Usiku Timu ya Yanga Imeshinda 6--0


Wachezaji wa Timu ya Yanga Afrika wanaoshiriki Kombe la Mapinduzi Cup wakiwa katika uwanja wa Amasan Zanzibar wakisubiri kukaguliwa na kuaza mchezo wao wa kwanza na Timu ya Jamuhuri uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Yanga Afrika imeshenda mchezo huo kwa bao 6-0.
Kikosi cha Timu ya Jamuhri kutoka Pemba kinachoshiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup, kilikubali kipigo cha bao 6-0 dhidi ya Timu ya Yanga Afrika mchezo uliofanyika usiku katika uwanja wa Amaan Zanzibar. Michuano hiyo ya Kombe la Mapinduzi inashirikisha Timu Tisa kutoka Zanzibar Uganda na Tanzania Bara.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Mzee Ali Haji akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Jamuhuri kabla ya kuaza kwa mchezo wao na Timu ya Yanga Afrika uliofanyika Uwanja wa Amaan usiku,

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Mzee Ali Haji akisalimiana na waamuzi wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi Kati ya Timu ya Yanga na Jamuhuri uliofanyika Uwanja wa Amaan.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Mzee Ali Haji akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Yanga Afrika kabla ya kuaza kwa mchezo wao na Timu ya Jamuhuri uliofanyika Uwanja wa Amaan usiku, 
Wachezaji wa Timu ya Jamuhuri wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Yanga kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup uliofanyika Uwanja wa Amaan Usiku.
Kikosi cha Timu ya Yanga African kinachoshiriki Kombe la Mapinduzi Cup kilichoaza michuano hiyo kwa ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Timu ya Jamuhuri kutoka Kisiwani Pemba mchezo uliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar usiku.
Kikosi cha Timu ya Jamuhuri kutoka Pemba kinashoririki Michuano ya Kombe la Mapinduzi CUP kilichokubali kipigo cha mabao 6-0 dhidi ya Timu ya Yanga African.  
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga African Msuva akijaribu kumpita beki wa Timu ya Jamuhuri wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika usiku katika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Yanga Afrika imeshinda kwa mabao 6-0. 


Wachezaji wa Timu ya Yanga wakishangilia bao lao la kwanza.katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi Cup mchezo uliofanyika usiku uwanja wa amaan Zanzibar. Golikipa wa Timu ya Jamuhuri akiwa na majozi baada kufungwa bao la sita na timu ya yanga wakati wa mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi Cup mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar usiku.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.