Naibu Waziri wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa
na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu, jijini Dar es Salaam
wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi katika Jeshi hilo leo. Masauni mara
baada ya kumaliza ziara yake aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya
Uhamiaji nchini, kuanzia sasa sare zote za askari na maafisa wa Idara hizo
zitashonwa katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa
maelekezo Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la
Magereza, Julius Chego (kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara katika
eneo la Ujenzi wa nyumba hizo 9,500, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo, ambazo
Rais Dk. John Magufuli ametoa Shilingi Bilioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba hizo. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Dk Juma Malewa
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa
suti) akikagua moja ya nyumba za askari wa Jeshi la Magereza zinazojengwa
Ukonga, jijini Dar es Salaam. Jumla ya nyumba 9,500 zinatarajiwa kujengwa
katika eneo hilo mara baada ya Rais Dk John Magufuli kutoa shilingi Bilioni
Kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Masauni alifanya ziara ya kikazi
katika maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo, na alitoa agizo kwa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji pamoja na Idara ya Uhamiaji, kuhakikisha kuwa, sare za idara hizo
kuanzia sasa zitakuwa zinashonwa katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga. Mbele
kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati)
akitoka katika Jengo la Useremala mara baada ya kukagua mashine mbalimbali
zinazotumika kuranda na kuchana mbao kwa ajili ya utengenezaji wa samani katika
Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa, na kulia ni Mkuu wa
Kiwanda hicho, Ismail Mlawa
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikiangalia
kikapu kilichoshonwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar
es Salaam. Masauni alifanya ziara katika kiwanda hicho na kujionea vitu
mbalimbali vinavyotengenezwa na wafungwa kiwandani hapo. Watatu kulia ni Kaimu
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa, kulia ni Mkuu wa
Kiwanda hicho, Ismail Mlawa
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
akiviangalia viti vilivyotengenezwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza
Ukonga, jijini Dar es Salaam, huku Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa akitoa maelezo
ya utengenezaji wa viti hivyo. Masauni alifanya ziara katika kiwanda hicho na
kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na wafungwa kiwandani hapo
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa
suti) akikiangalia kitanda kilichotengenezwa na wafungwa katika Kiwanda cha
Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam, huku Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa
(kushoto) akitoa maelezo ya utengenezaji wa kitanda hicho. Masauni alifanya
ziara katika kiwanda hicho na kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na
wafungwa kiwandani hapo. Wapili kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza nchini, Dk Juma Malewa
Naibu Waziri wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiiangalia moja ya nguo
iliyoshonwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es
Salaam, huku Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa (kulia) akitoa maelezo ya
utengenezaji wa nguo hiyo. Masauni alifanya ziara katika kiwanda hicho na
kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na wafungwa kiwandani hapo. Kushoto
ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment