Habari za Punde

Timu ya Simba Imefanikiwa Kuingia Nusu Fainali Baada ya Kuifunga Timu ya Jangombe Boys kwa Mabao 2--0.

Mshambuliaji wa Timu ya Simba Juma Liuzio akimpita mchezaji wa timu ya Jangombe Boys Abdi Kassim wakatin wa mchezo wao wa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa kundi B Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan jioni.
Katika mchezo huu timu ya Simba imeweza kutoka kifua mbele baada ya kuifunga Timu ya Jangombe Boys, kwa mabao 2--0. na kuchukua nafasi ya kwanza katika kundi hilo na kukutana katika mchezo wa Nusu fainali ma mshindi wa Kundi A Timu ya Yanga baada ya jana kufunga na timu ya Azam kwa mabao 4-0. 
Mchezo wa Yanga na Simba kufanyika siku ya Jumanne usiku  na jioni itakuwa kati ya Timu ya Azam na mshindi katika ya Timu ya Taifa ya Jangombe na URA Unaofanyika usiku huu. 
Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Katika mchezo wa jioni uliozikutanisha timu za Simba na Jangombe Boys, mchezo uliokuwa wa upande mmoja timu ya Simba imemiliki mpira muda mwingi wa mchezo na kujipatia bao la kwanza katika dakika 12 ya mchezo kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Laudit Mavugo. hadi mapumziko timu ya Simba ikiwa mbele kwa bao moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi golini kwa Timu ya Jangombe Boys na katika dakika ya 54 ya mchezo kipindi hicho timu ya Simba ikaandika bao la pili kupitia mshambuliaji wake Laudit Mavugo tena.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.