Habari za Punde

Wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu waaswa kutowafungia ndani watoto

Na Salmin Juma , Pemba

Ingawa juhudi zinaendelea kufanywa na wadau wenye kushughulika na watu wenye ulemavu wakiwamo Kituo cha huduma za sheria ZLSC kwa kuwasomesha na kuwahamasisha wazazi na walezi wa watu wenye ulemavu kutowafungia ndani watoto wao, lakini bado hali inaonekana haijarekebishika  jambo linalopelekea kuzidi kuathirika kisaikolojia kwa  watu wa aina hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi  jana  kwa njia ya simu kutoka Hounslow London Uingereza  baba wa mtoto mwenye ulemavu Faria Shawwal Zam ambae pia ni mratibu wa jumuiya ya Hilmy Disability Charity Organization inayoyofanyia kazi zake za ugawaji misaada kwa wenye ulemavu visiwani Zanzibar amesema kua, tokea kuanza kwa shuhuli ya kuwasaidia watu hao katika visiwa vyote vya Pemba na Unguja amegundua kua watu hao wanakosa haki zao za msingi kutokana na baadhi ya wazazi na walezi kutoelewa  umuhimu  wa kuwatoa nje watoto hao na badala yake huwafungia ndani kwa kukimbia aibu.

Amesema kua watu hao ni binaadamu wa kawaida na wanastahiki kutolewa nje ili wajumuike na wenzao kwani kujumuika huko kunasaidia kukua katika mfumo wa akili.

Zam  amefahamisha kua ni vyema kwa wazazi na walezi wa watoto hao kutoona aibu kuwatoa nje kwani hizo ni kadari zake MUNGU na hakuna kuona aibu kupata mtoto kama huyo na endepo wakiwatoa  faida za kimaendeleo wataanza  kuziona kapitia matendo ya watoto hao.

Katika hatua nyengine Zam  amesema, bado hali ni ya kusikitisha kwa watu hao nchini Zanzibar kwani wanaonekana kua  wametengwa na huduma nyingi hukosa kutokana na kutojaliwa na jamii iliyowazunguka.

Sambamba na hayo amewataka wenye kijiweza kuichumi na hata wa kipato cha kawaida na wa chini kuiunga mkono taasisi ya Hilmy Charity inayotembelea watu wenye ulemavu Zanzibar na kuwapatia zawadi ya vigari maalum huku akisema kua bado taasisi hiyo inaendelea kutafakari juu ya kuwasaidia wenye ulemavu wa aina tofauti kama wale wasioona na wengineyo.

Kwa upande wake Mratibu wa kituo cha huduma za sheria afisi ya Pemba Bi Fatma Khamis Hemed hivi majuzi akiwa na wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu katika ukumbi wa kituo hicho Chakechake amesema kuwambia wazazi hao wawe na tabia za kuwatoa nje watoto badala ya kuwafungia ndani kwa kuogopa aibu.

Alisema watoto wenye ulemavu ni wa kutunzwa na kuhifadhiwa vizuri kwani wanavipaji na wanaweza kufanya mambo mazuri na kila mmoja akapendezewa na jambo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.