Habari za Punde

Bodi ya Mapato Tawi la Pemba Wakabidhi Vifaa Kwa Ajili ya Hospitali ya Wete.

Afisa Mdhamini wa Bodi ya Mapatoa Zanzibar (ZRB) Tawi la Pemba,Ndg.Said Ali Mohamed (kushoto) akimkabidhi mashuka 50 Katibu Afisa Tawala wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,Ndg.Ahmed Khalid Abdalla (kulia) akipokea kwa niaba ya Wizara ya Afya kwa hospitali ya Wilaya ya Wete Pemba hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika hospitali ya Wete Pemba. 
Afisa Mdhamini wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Tawi la Pemba,Ndg.Said Ali Mohamed akikabidhi magodoro 50 kwa Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Pemba. kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya Wete Pemba.
Afisa Mdhamini wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB)Tawi la Pemba,Ndg Sail Ali Mohammed akipokea shukrani kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wete Dk Mbwana Shoka Salum, kwa msaada wao huo walioukabidhi kwa hospitali ya Wete Pemba kwa matumini ya Wananchi wanaofika hospitalini hapo kupata huduma za matibabu.

Maofisa wa Bodi ya Mapato Tawi la Pemba wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya Wodi za hospitali ya Wete Pemba. ,wakiwa pamoja na Meneja wa bodi hiyo katikati Said Ali Mohamed, baada ya kukabidhi msaada kwa Uongozi wa Serikali ya Mkoa na Wizara ya Afya

Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.