Habari za Punde

Hafla ya kuwakabidhi vyeti wafanyakazi bora wa viwanja vya ndege


  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar, Muhidin Talib, akizungumza neno na dhamira ya kufanya hafla kwa Wafanyakazi wa viwanja vya ndege  kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, Abdulghani Msoma , ili kuzungumza na Wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Karume Pemba, katika hafla ya kuwakabidhi vyeti na fedha taslim Wafanyakazi bora kwa mwaka 2016/2017.
 Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar,Abdulghani Msoma , akimkabidhi Cheti na zawadi mmoja wa Wafanyakazi bora wa Kiwanja cha ndege cha Karume Pemba, ambao walifanya vyema katika utekelezaji wa majukumu yao kwa mwaka 2016/2017.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar, Abdulghani Msoma, akionesha Chaeti ambacho amevikabidhi kwa Wafanyakazi wa bora  wa Kiwanja cha ndege cha Karume Pemba.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar , Abdulghani Msoma, akizungumza na Wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Karume Pemba, mara baada ya kuakbidhi zawadi na vyeti kwa Wafanyakazi
hao ambao walifanya vyema katika kutekeleza majukumu yao kwa mwaka 2016/2017.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar, Abdulghani Himid Msoma , akionesha Katiba ya Zanzibar , juu ya vipengele vinavyotowa haki kwa Wafanyakazi katika kujiunga na vyama vya Wafanyakazi na mambo mengine  huko katika kiwanja cha ndege cha karume Pemba.

 Makamo Mwenyekiti wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, Hamad Bakar Mshindo, akiwapa Wasia Wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Karume Pemba Pemba juu ya kuipenda kazi yao kwani Kazi ndio kipimo cha
utu , sambamba na kujiendeleza Kielimu , mara baada ya hafla ya kuwakabidhi vyeti na Zawadi Wafanyakazi bora waliofanya vyema katika kutekeleza majukumu yao kwa kipindi cha mwaka 2016/2017.Baadhi wa Wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Karume Pemba , wakiwa katika mkutano wa hafla ya kuwakabidhi Zawadi Wafanyakazi bora wa kiwanja cha ndege cha Karume Pemba.

Picha zote na Bakar Mussa-Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.