Habari za Punde

Ujumbe wa Wadi ya Makunduchi Waendelea na Ziara Yao Nchini Sweden.

Mjumbe wa Wadi ya Makunduchi ndugu Mohamed Muombwa (hayupo kwenye picha) alihudhuria mafunzo ya wafuga nyuki wa Manispaliti ya Sundsvall. Somo lililotolewa ni umuhimu wa kupanda maua wanayopenda nyuki Karibu na mizinga ya nyuki.
Diwani wa Wadi ya Makunduchi bi Zawadi alimkabidhi pia bwana Pinheiro mwenyekiti wa Kamari ya Elimu ya Baraza la Manispaliti zawadi ya pilipili manga kwa ajili ya kutangaza viungo vya Zanzibar nchini Sweden
Sheha mstaafu wa shehia ya Mzuri Kaja mwalimu Mwita Masemo akibadilishana mawazo na mwalimu wa uchoraji ndani ya jengo la Manispaliti ya Sundsvall ambamo ndani yake mlikuwa na maonyesho ya kazi za Sanaa.

1 comment:

  1. Very good Lakini napenda kuuliza, hivi wanaokwenda huko huwa hawabadiliki? Kila mwaka ni hao hao au vipi. Hongera Wana Makunduchi

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.