WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO
YA AMALI INATANGAZA NAFASI ZA MASOMO ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI YA MAURITIUS,
NGAZI YA SHAHADA YA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2017-18
1 Sifa za muombaji
Asiyezidi miaka 25
Awe
amemaliza kidato cha sita na amefaulu daraja la kwanza au la pili au amehitimu
ngazi ya Diploma.
2 Utaratibu wa malipo
Waombaji watakao bahatika
kupata nafasi hizo watapatiwa malipo yafuatayo;
i. Posho la kila mwezi
Rs 8,300 kwa USD 266
ii.
Ada ya masomo Rs
100,000 kwa USD 3205 kwa mwaka
iii.
Tiketi kwa kipindi
chote cha masomo hadi kumaliza.
3 Njia za kufanya maombi Waombaji wote wanatakiwa waombe barua
ya kujiunga na chuo (Admission Letter) kupitia mitandao ya vyuo vya Mauritius
kama vifuatavyo;
CHUO ANUANI
University of Mauritius www.uom.ac.mu
University of Technology,
Mauritius www.utm.ac.mu
Universities des
Mascareignes www.udm.ac.mu
Fashion & Design
Institute www.fdi.ac.mu
Mauritius Institute of
Education www.mie.ac.mu
Mahatma Gandhi Institute www.mgirti.ac.mu
Rabindranath Tagore Institute
www.mgirti.ac.mu
Fomu ya maombi na maelekezo
yake inapatikana katika mtandao ufuatao;
http://ministry-education.govmu.org/English/Scholarships/ Pages/default.aspx
4. Utaratibu wa kuwasilisha maombi Waombaji wa nafasi hizo
watatakiwa kuwasilisha viambatisho vifuatavyo katika maombi yao;
1 Cheti cha kuzaliwa
2 Vivuli vya Vyeti vya
kumalizia masomo vya “O” na “A” Level
3 Fomu ya Afya (Medical
Report)
4 Kivuli cha pasi ya
kusafiria
5 Nyaraka zote zinahusiana
na masomo anayotaka kusomea
Kwa maelezo zaidi Kuhusiana
na nafasi hizo fika; Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali – Kitengo cha Uratibu
wa Elimu ya Juu chumba No.57.
No comments:
Post a Comment