Habari za Punde

Mchezo Maalum wa Kumuaga Aliyekuwa Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe Ninja.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Kesho Ijumaa ya June 23, 2017 Saa 3:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan Mlinzi mpya wa Yanga Abdallah Haji Shaibu "Ninja" atawaaga Mashabiki wake katika mchezo maalum kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi Mlandege SC mchezo ambao pia ni wa uzinduzi wa COCO SPORTS NDONDO CUP.

Ninja amesajiliwa Yanga wiki iliyopita akitokea Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar ambapo amefunga mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo na kesho atapata fursa kubwa ya kuwaaga Mashabiki wake.

Kiingilio katika mchezo huo ni Shilingi Elfu 2000/=, 3000/=  na VIP 5000/=.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.