Habari za Punde

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zuberi Aipongeza Timu ya Taifa ya Riadhaa U -18

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid aipongeza Timu ya Taifa ya Riadhaa ya Zanzibar U - 18, kwa kufanya vizuri katika ya Zone 5 ya Afrika Mashariki na Kati yaliofanyika Jijini Dar es Salaam na kuchukua nafasi ya Tatu kwa Jumla na kushika nafasi ya kwanza kwa Wanaume,akitowa pongezi kwa timu hiyo na kutimiza ahadi yake ya kuizawadia ikifanya vizuri michuano hiyo hafla hiyo imefanyika katika ukumbi mdogo wa Baraza chukwani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe. Chuom Kombo Khamis akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuwapongeza vijana hao kwa ushindi wao huo na kuonesha uwezo wao.
Mwakilishi wa jimbo la Kikwajuni na Meneja wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Mhe.Nassor Salum Jazira akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuwapongeza vijana hao waliofika kutambulishwa kwa wajumbe kwa ushindi wao.
Wanamichezo wa Timu ya Taifa ya Riadhaa ya Zanzibar U - 18. wakifuatilia hafla hiyo ya kupongezwa na kukabidhiwa fedha na Spika Mhe. Zuberi kwa kutimiza ahadi yake wakati walipofika kumuanga.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Riadhaa Zanzibar Makame Mshinda akito neno la shukrani kwa niaba ya uongozi wakati wa hafla hiyo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid akikabidhi fedha alizoahidi kwa Vijana wa Timu ya Taifa ya Zanzibar ya Riadhaa kwa kiongozi wa Timu hiyo Suleiman Ame.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.