Habari za Punde

Ugeni wa Dkt. Ramakrishna Sithanen aliyekuwa waziri wa Fedha na Naibu Waziri Mkuu Mauritius

 Mkurugenzi wa Pennyroyal(Gibraltar) Zanzibar Ltd na Zanzibar Amber Resort Bw. Saleh Mohammed Said akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa ugeni muhimu wa aliyekuwa waziri wa Fedha na Naibu Waziri Mkuu Mauritius Dkt. Ramakrishna Sithanen anaetarajiwa kuwasilin tarehe 06 Juni


Jumanne tarehe 6 Juni, aliyekuwa waziri wa Fedha na Naibu Waziri Mkuu Mauritius Dkt. Ramakrishna Sithanen anategemewa kuwasili Zanzibar kwa  mualiko wa Mkurugenzi wa Pennyroyal (Gibraltar) Zanzibar Ltd na Zanzibar Amber Resort Bw. Saleh Said.

Dkt. Ramakrishna Sithanen anatarajia kukutana na wajumbe 40 wa Zanzibar Association of Tourism (ZATI), Zanzibar National Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (ZNCCIA), Zanzibar Association of Tour Operators (ZATO) katika hoteli ya Serena tarehe 7 Juni, na watazungumza maswala mbalimbali ikiwemo jinsi ya kubadilisha na kuboresha utalii Zanzibar. Pia atakutana na viongozi wa serekali ya Zanzibar. Ajenda kuu ya Mkutano huo ni “Kuondoa Umasikini Zanzibar Kupitia Uwekezaji wa Kigeni.”

Pennyroyal Gibraltar Ltd ilichukua uamuzi wa kumwalika Zanzibar Dkt. Ramakrishna Sithanen, kwa sababu ya ujuzi na weledi wake kwa kuwa kiungo kikuu cha mabadiliko ya Mauritius. Ni mategemeo ya Saleh kwamba, Zanzibar itafuata nyao za Mauritius katika kupunguza umasikini na kukuza uchumi kupitia Utalii. 

"Naamini tukifanya kazi pamoja na Dkt. Sithanen na kupata ujuzi wake, kampuni yetu na Zanzibar kwa ujumla tutafanikisha kulete mabadiliko ya kimaendeleo kwa sababu ana uzoefu mkubwa, na amewezesha Mauritius kupata mafanikio. Ninayo furaha kwamba amekubali kuja kutuelimisha na kutupa ujuzi wake, na wadau wa utalii na maendeleo wanasubiri kwa hamu kupata kusikia kutoka kwa mtaalamu huyu aliyebobea katika maswala ya uwekezaji na Utalii." Alisema Mkurugenzi wa Pennyroyal Gibraltar Zanzibar Ltd Saleh Said.

Dkt. Ramakrishna Sithanen ana uzoefu wa miaka 37 katika sekta binafsi kama mwana uchumi na ameshawahi kushikilia nafasi za juu kama Mkurugenzi kwenye Shirika la Ndege Mauritius, Mkurugenzi wa Mikakati kwenye Benk ya maendeleo ya Africa (African Development Bank) na alikua Mshauri wa Kimataifa katika Afrika na nchi za Bahari ya Hindi.

Mwaka 1991 alipata nafasi ya kua Waziri wa Fedha Mauritius mpaka 1995, kipindi hicho alifanikiwa kubadilisha sera za kiuchumi nchini Mauritius na kupanua uchumi wa nchi. Alichaguliwa kama Naibu Waziri Mkuu mwaka 2005 na kuleta mabadikilo yakijasiri katika mataasisi mbalimbali nakufanikiwa kukuza uchumi nchini humo.


Zaidi ya hapo mwaka 2009 alipata heshima ya juu kutoka kwa Raisi wa Mauritius inayo julikana kama Grand Commander of the Order of the Star and Key. Dkt. Sithanen anasifika kwa kazi nzuri aliyofanya na mafanikiyo ya kukuza uchumi wa Mauritius, kwa sasa ni Mwenyekiti na Mtokea 2013kurungezi wa International Financial Services, ambayo ni moja wapo ya makampuni makubwa yanayo simamia fedha Mauritius. Vilevile ni Mwenyekiti wa Bodi ya maendeleo ya Rwanda na alikuwa Mshauri wa Serikali ya Rwanda kwa mambo ya kodi, ushindani na Fedha baina ya mwaka 2013 na 2015.


"Ni mategemeo yetu kuwa, safari hii ya  Dkt. Ramakrishna Sithanen hapa  italeta  mafanikio makubwa sana kiuchumi hasa hasa kenye sekta ya utalii Zanzibar, na sisi tutapata kujua vigezo vilivyo wezesha Mauritius kufanikiwa. Dkt. Sithanen anauelewa mzuri wa changamoto zinazo kabili uchumi wa Afrika na visiwa vidogo kama Zanzibar, ni matumaini yangu kwamba serikali ya Zanzibar itapata muamko wa mabadiliko" Alisema Saleh Said


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.