Habari za Punde

Unguja Noma Michezo ua Umiseta Mwanza. Kila Siku Hutowa Dozi Leo Wamchapa Mtu 5 - 0.

Na Abubakar Kisandu Mwanza.
Wakicheza mchezo wa tatu Timu ya soka ya Unguja imeendelea kuwapa raha wana Mwanza kufuatia ushindi wake wa tatu mfululizo baada ya asubuhi ya leo kuwapiga timu ya Mara mabao 5-0 kwenye Mashindano ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba mkoani Mwanza.

 Mabao ya Unguja yamefungwa na Ali Hassan “Ndimbo” (2), Walid Abdi “Pato”, Faki Kombo na Mundhir Abdallah “Diarra”.
 Kwa matokeo hayo Unguja ndio kinara akiwa na alama 9 wapo kundi “C” lenye jumla ya timu 7 ambapo wapo pamoja na Katavi, Kagera, Mara, Mbeya, Iringa na Dar es salam.

Mchezo mwengine Unguja watacheza kesho Jumapili June 11, 2017 saa 12:30 za asubuhi dhidi ya Mbeya, kisha Jumatatu June 12, 2017 Unguja dhidi ya Iringa, Jumanne June 13, 2017 Unguja watamalizana na Dar es salam.

Michezo mitatu ya awali Unguja waliifunga Katavi 4-0, wakaichapa Kagera 3-0 na leo wakaipiga Mara 5-0, hivyo wameshafunga jumla ya mabao 12 katika michezo 3 wakati lango lao bado halijaonjwa hata bao moja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.