Habari za Punde

Unguja yawa gumzo Mwanza yawachapa Kagera3-0

Na. Abubakar Khatibu "Kisandu"
Timu ya soka ya Unguja imeendelea kuwa gumzo jijini Mwanza kufuatia ushindi wake wa pili mfululizo baada ya asubuhi ya leo kuwachapa Kagera mabao 3-0 kwenye Mashindano ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba mkoani Mwanza.

Nyota wa mchezo huo ni Walid Abdi (Pato) alipiga hat trick na ndio bao lake la nne katika Mashindano hayo kufuatia jana kufunga bao moja walipoichapa Katavi 4-0.

Huo ni mwendelezo mzuri kwa vijana hao wa Unguja ambapo mpaka sasa wakiwa kinara wa kundi lao C kwa alama zao 6 kufuatia kushinda michezo yote miwili na pia wana jumla ya mabao 7 ya kushinda wakati lango lao linaloongozwa na Mlinda mlango hatari Aley Suleiman “Manula” halijaruhusu kufungwa hata bao 1.

Pia katika michezo hiyo miwili waliyocheza Unguja wameshafunga jumla ya Hat trick mbili kufuatia leo Walid Abdi (Pato) kufunga na jana Mundhir Abdallah (Diarra) kupiga.

Mchezo mwengine Unguja watacheza na Mara Siku ya Jumamosi ya June 10, 2017, kisha kucheza tena Jumapili June 11, 2017 dhidi ya Mbeya, Jumatatu June 12, 2017 Unguja dhidi ya Iringa, Jumanne June 13, 2017 Unguja watamalizana na Dar es salam.

Unguja ndio kinara akiwa na alama 6 wapo kundi “C” lenye jumla ya timu 7 ambapo wapo pamoja na Katavi, Kagera, Mara, Mbeya, Iringa na Dar es salam.

KIKOSI CHA UNGUJA KILICHOPO MWANZA KATIKA MASHINDANO YA UMISSETA

WALINDA MLANGO
Aley Ali Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu)
WALINZI
Ibrahim Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi (Glorious), Abubakar Khamis (Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali Issa Omar (Lumumba),  Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki) na Abbas Yahya.
VIUNGO
Amani Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess” (Lumumba), Haji Suleiman (JKU Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku “Ozil” (Kinuni) na Eliyasa Suleiman (K-pura).
WASHAMBULIAJI
Faki Kombo (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan (Bububu), Walid Abdi “Pato” (Mwera), Ali Mohd Seif (Tumekuja) na Ali Omar (Mwera).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.