Habari za Punde

AZAM TV Yatua Kisiwani Pemba Kurusha Matangazo ya Tamasha Pemba Bonaza Weekend.


Drones” kutanda anga
Nikwa ajili ya Matangazo Mubashara kutoka PBA
Kuanza rasmi Alhamis 27 Julai saa 4:00 asubuhi kwa mkutano na wa wanahabari
Kati ni Yussuf Hamad mwenyekiti wa kampuni ya Rafiki Network akizungumza na manahodha wa Ngalawa pamoja na waendesha baiskeli watakaoshiriki  katika tamasha la Kimichezo kisiwani Pemba “Pemba Weekend Bonanza” Kulia ni Salim Jabu Dawa Mratibu wa Matukio Kisiwani Pemba na Kushoto ni Umrat Khator Khamis ambae ni Afisa Masoko wa  Kampuni ya Rafiki.

Ali Othman Ali

Timu ya AZAM TV imewasili rasmi kisiwani Pemba kwa ajili ya kurusha “live” Tamasha la Kimichezo Kisiwani Pemba lilioandaliwa na Kampuni ya Rafiki Network.

Akizungumza  kwa njia ya simu mara baada ya kuwasili Azam Sea Link 2 bandari ya mkoani Raisi wa Kampuni Ya Rafiki Network Bw. Hamad Omar Hamad amesema amefarijika kusikia AZAM wamewasili na vifaa vyakisasa zikiwemo drones ambazo zita paa angani kuhakikisha kwamba matukio yote yanaonekana ndani na nje ya nchi.

Nae Mwenyekiti wa Kampuni ya rafiki Network Bw. Yussuf Shoka Hamad amewataka manahodha na waendesha baiskeli ambao watashiriki katika Bonanza kujali sheria za michezo hiyo wakiamini kwamba Kampuni ya Rafiki Network nia yake ni kuibua vipaji vyao na kuviendeleza kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

“Tumeanzisha Tamasha hili la Pemba Weekend Bonanza ili kuibua vipaji vitakavyotuwakilisha katika medani za kitaifa na kimataifa Hivyo tunawaomba kujali sheria na kanuni za michezo mukijua kwamba mashindano yote yanaoneshwa mubashara na Kituo cha TV cha AZAM” amesema bwana Hamad.

Tamasha la Pemba Weekend Bonanza Litaanza rasmi siku ya Ijumaa 28 Jula 2017 saa nane jioni Kwa mchezo wa Ng’ombe utakaofanyika Skuli ya Chwale ambapo siku ya Jumamosi tarehe 29 Julai itakua ni mashindano ya baiskeli hatuo ya mchujo.

Bonanza litaendelea Siku ya kilele kwa shangwe na shamra shamra za ngoma mbalimbali huko katika fukwe za vumawimbi ambako mashindano ya kuogelea pamoja na mchuano mkale wa kihistoria wa resi za ngalawa utafanyika


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.