Habari za Punde

MADUNDO APANIA KUPANDA TENA DARAJA TIMU YAKE YA VILLA UNITED

Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.
Baada ya kufanikiwa kupanda daraja la kwanza Taifa msimu ulopita Timu ya Villa United “Mpira Pesa” yenye Maskani yake Mwanakwerekwe imepania na msimu huu mpya kuondoka daraja hilo na kupanda daraja jengine.

Akizungumza na Mtandao huu kocha mkuu wa timu hiyo Ramadhan Abdulrahman “Madundo” amesema kwa soka la Zanzibar lilivo hawana sababu timu yao isipande tena daraja msimu huu kama ilivyofanya miaka miwili mfululizo iliyopita.

“Sisi kila mwaka tunapanda daraja jengine sasa sioni sababu na mwaka huu tusipande daraja jengine, kwani nina wachezaji wenye uwezo binafsi na pia uongozi wangu upo imara”. Alisema Madundo.

Timu ya Villa United ilianzishwa mwaka 2013 ambapo ilianzia kucheza madaraja ya Vijana Wilaya ya Mjini lakini ilipofika msimu wa mwaka 2015-2016 ilishiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini na kufanikiwa kupanda daraja, Msimu ulopita wa mwaka 2016-2017 Villa ilifanikiwa tena kupanda daraja la Kwanza Taifa ambapo msimu ujao mpya wa mwaka 2017-2018 pia wamepania kupanda daraja jengine kama ni ligi 2 au ligi kuu soka ya Zanzibar itategemea msimu huu mfumo gani utatumika kwenye madaraja husika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.