Habari za Punde

Kipidwa Cup Kuanza Jumamosi Hii Hapa Ratiba ya Makundi.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mashindano ya Ndondo ya KIPWIDA CUP yanatarajia kuanza rasmi Jumamosi July 8, 2017 kwenye uwanja wa Lion kids huko Maungani ambapo watazindua kati ya Big Nation dhidi ya Kisaka saka saa 10:00 za jioni.

Akizungumzia matayarisho ya Mashindano hayo mratibu Abdul Rahim Kipwida amesema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri ambapo mwaka huu Bingwa atapatiwa Zawadi ya Ng’ombe huku mshindi wa pili atazawadiwa Mbuzi Mnyama.

“Maandalizi yamekamilika tunasubiri ifike Jumamosi tu, mwaka huu Bingwa atapata Ng’ombe na wa pili tutampatia Mbuzi, lakini zawadi zitaongezeka zaidi ya hizo”. Alisema Kipwida.


Katika Mashindano hayo mwaka huu kuna makundi manne (4), kundi “A”, “B”, “C” na “D”.
KUNDI “A”
Big Nation, Kisaka saka, Basra Boys na Mpira Pesa
KUNDI “B”
African Sports, Lakidatu, Red Scorpion na Kisaka saka Boys
KUNDI “C”
Lion Kids, Umoja Star, Njaa Kali na Polisi Mazizini
KUNDI “D”
Chilla All Star, Mtoko Pensi, Top Life na New Manter.
RATIBA YA MZUNGUKO WA KWANZA
Jumamosi July 8, 2017 Big Nation v/s Kisaka saka
Jumapili July 9, 2017 Basra Boys v/s Mpira pesa
Jumatatu July 10, 2017 African Sports v/s Lakidatu
Jumanne July 11, 2017 Red Scorpion v/s Kisaka saka Boys
Jumatano July 12, 2017 Lion Kida v/s Umoja Star
Alhamis July 13, 2017 Njaa kali v/s Polisi Mazizini
Ijumaa July 14, 2017 Chilla All Star v/s Mtoko Pensi
Jumamosi July 15, 2017 Top life v/s New Manter

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.