Habari za Punde

Muonekano iwa Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Muonekano wa Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba baada kukamilika kwa ukarabati wake uliochukuwa muda kwa uwekaji wa Tartan na Nyasi za Bandia katika Uwanja huo, na hatimai kukamilika kwa utiaji wa rangi katika majukwaa ya watazamaji. 

Kwa sasa uwanja huo umekuwa katika muonekano wa Uwanja wa Kimataifa na kuweza kufanyika michezo yoyote ile ya Kimataifa katika uwanja huo kama unavyoonekana ukiwa katika haiba ya kupendeza.

 Kwa sasa unahitaji bao la matangazo ya mchezo wakati yakifanyika mashindano katika uwanja huo.   (Picha na Abdi Suleiman Pemba.)
Sehemu ya kibanda cha kuoneshea matango wakati mchezo ukifanyika kinahitaji kufanyiwa matengenezo kwa kuwa cha kisasa zaidi.

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.

WADAU wa Soka Kisiwani Pemba, wamesema ipo haja ya Uwanja wa Gombani Kuwekewa bao la Matokeo (skoobord) la kisasa, baada ya uwanja huo kufanyiwa ukarabati wa hali ya Juuu.

Wamesema sasa uwanja ukipatiwa bao hilo la matokeo utakuwa wa kisasa zaidi, kufuatia kuwekewa nyasi bandi, raba ya kukimbilia, upakaji wa rangi katika majukwa na kujengwa upya kipaa cha eneo la VIP.

Walisema ili kutimiza hadhi itakayokuwemo uwanjani hapo, skoobord iliyopo sasa inapaswa kuondolewa kwani haiyendani na hadhi ya uwanja huo ulivyo hivi sasa.

Khamis Juma Said alisema kukamilika kwa kazi ya upakaji wa rangi ndani ya Uwanja huo, umeirudisha upya hadhi ya uwanja wa ngombani tokea ulipomaliza kutengenezwa na wakorea.

“Sasa utakuwa uwanja wa kisasa, ni Vizuri Dk Shein kutupia jicho katika kutengeneza Skoobord ya kisasa ya kiyoo itakayoendana na hadhi ya sasa”alisema.

Ali Nassor Othman aliwataka viongozi wa Uwanja huo, kuhakikisha wanautunza na kuuthamini kwa kuweka walinzi kila pahala kuhakikisha rangi haichunwi iliyopo.

Alisema baada ya kumalizika kwa kazi ya Upakaji wa Rangi, kazi inayofuta kuzibwa katika baadhi ya milango ambayo watu wanapenye na kuifanyia ukarabati milango ambayo viyoo vilivunjika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.