Habari za Punde

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                                                                          25.07.2017
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amerejea nchini leo akitokea nchini Uingereza.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali pamoja na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walimpokea Dk. Shein wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

Dk. Shein katika safari hiyo maalum ya nchini Uingereza, alifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Watendaji wengine wa Serikali.

 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.