WASANII kutoka Kampuni ya Jufe
Production wakioongozwa na Mwinyi mpeku, wakionyesha igizo la namna ya watu
wanavyoyamaliza kesi za ubakaji nje ya vyombo vya sheria, kabla ya kuanza kwa
mkutano wa wazi wa kuelezwa wananchi umuhimu wa kushiriki na kushirikishwa
wakati wa utungaji wa katiba na sheria, mkutano huo ulifanyika shehia ya Tumbe
Mashariki, wilaya ya Micheweni Pemba
MRATIBU wa Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akijibu maswali ya
wananchi wa shehia ya Tumbe mashariki wilaya ya Micheweni, kweye mkutano wa
wazi wa kuelezewa umuhimu wa wananchi kushiriki na kushirikishwa, wakati wa
utungaji wa Katiba na sheria
NAIBU
sheha wa shehia ya Tumbe Mashariki wilaya ya Micheweni, Seif Omar Hamad,
akimtambulisha Msaidizi wa sheria Jimbo la Tumbe kwa wananchi wa shehia hiyo, waliohudhurai
mkutano wa wazi wa kuelezwa umuhimu wa ushirikishwaji na ushiriki, wakati wa
utungaji wa sheria na katiba, mkutano huo ulitayarishwa na Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba
WASANII kutoka Kampuni ya Jufe
Film Producation ya mjini Wete, wakipamba jukwaa kwa kucheza musiki wa kizazi
kipya, kabla ya kuanza kwa mkutano wa wazi wa kuelezwa umuhimu wa
ushirikishwaji na ushiriki wakati wa utungaji wa sheria na katiba, kwa wananchi
wa shehia ya Tumbe Mashariki wilaya ya Micheweni Pemba, mkutano huo
ulitayarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba
No comments:
Post a Comment