Ramallah, 20/09/2017 Donia Al-Watan: Rais wa Palestina “Mahmoud Abbas” amesisitiza kuwa uhuru wa nchi yake upo karibu hauepukiki na kwamba
uvamizi wa Israeli unafikia mwisho, akisema: "Aidha upatikane uhuru au
haki kamili ya wote katika nchi ya Palestina ya kihistoria."
Rais Abbas Jumatano
jioni akihutubia Mkutano wa 72 wa Umoja wa Mataifa, ameongeza kusema kwamba, imepita miaka ishirini na minne
tangu kusainiwa kwa Mikataba ya mpito ya Oslo, ambayo ilionesha ukomo wa
uvamizi wa Israeli na kuwapa matumaini Wapalestina, ya kuanzishwa kwa Dola yao
huru, huku akihoji " Tuko wapi sasa na matumaini haya?."
Amesema:"Tumekubali
uwepo wa Dola ya Israeli kupitia mipaka
ya mwaka 1967, lakini Israeli kutokubali uwepo wa Dola ya Palestina kunatupa
maswali mengi. Badala ya kuzingatia sababu, inafanya juhudi kuteka misimamo ya kimataifa
kwa masuala yasiyo na uzito wowote, yatokanayo na sera zake za kikoloni.
Tunapoitaka na kutakiwa na jumuiya ya kimataifa kukomesha uvamizi wake, inadai
ni uchochezi na kukosekana ushiriki wa
Palestina na kuwekwa kwa masharti yasiyowezekana."
Rais Abbas ameongeza
kusema kuwa,anaelea machafuko ni Utawala wa kivamizi wa Israeli katika ardhi
yetu,uvamizi ambao umefikia zaidi ya nusu karne,huku zaidi ya miaka kumi sasa
tumekubaliana kuunda kamati ya pande
tatu ambazo ni Marekani,Israeli na Palestina, ili kumaliza suala la uchochezi.Kamati imefanya kazi kwa muda, lakini tumekuwa
tunatoa wito wa kufufuliwa wa kamati hiyo hatupati mrejesho. Hivi ni nani
anaekaribisha hilo na kufanya juhudi ya kulifanya liwepo?.
Amesema
pia,kuendelea kwa uvamizi ni aibu kwa Israeli na Jumuiya ya Kimataifa,ni wajibu
wa Umoja wa Mataifa kumaliza uvamizi huo ili kuwezesha jamii ya Palestina
kuishi kwa uhuru na ustawi katika ardhi yake,huku mji mkuu wake ukiwa ni Jerusalemu
ya Mashariki."Kukomesha uvamizi na vitendo vyake vya kidhalimu, vitakuwa
na athari kubwa mno katika kupambana na udaidi pia mashirika yake kukosa
karatasi muhimu ambazo huzitumia kwa kuuza fikra zao."Tunatilia mkazo la
kukaliza uvamizi ili kukamilisha juhudi zetu katika kukabiliana na mashirika
hayo ya kigaidi,kwani Wapalestina wapo dhidi ya ugaidi wa ndani,kikanda na wa
kimataifa.
"Tuliwasilisha
mpango wa amani wa Kiarabu unaoitaka
Israeli kuondoka katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu tangu mwaka 1967 lakini Israeli haikujibu,kama
ilivyoufanyia ule mpango ujulikanao kama “Road Map” uliowasilishwa na pande nne
na kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,hali inayoonekana kana
kwamba Israeli ipo juu ya sheria. Vilevile ukaja mpango wa amani wa Ufaransa
ukifuatiwa na mkutano husika mjini Paris,lakini juhudi zote hizi zilikataliwa
na kupigwa na Israeli."
Ameongeza
kusema:”Tulimuomba Waziri Mkuu wa Israeli akubali ufumbuzi wa dola mbili, kisha
tukae kuzungumzia suala la mipaka akakataa,licha ya jitihada zetu kufikia amani
ya kweli, lakini Israeli inaendelea kuvuruga na kuendeleza ujenzi wa makazi ya
walowezi Ukingo wa Magharibi na kila mahali, hatimae hakuna tena nafasi kwa
ajili ya taifa la Palestina."Vitendo viovu vya Israeli katika mji mtakatifu,
vitachochea hisia za uadui wa kidini, ambao unaweza kugeuka mgogoro mkubwa wa
kidini, tumeiomba serikali ya Israeli kuheshimu sheria na historia ya sehemu
hizo takatifu lakini Israel tangu ilipoikalia kimabavu Jerusalemu mwaka 1976,
imekuwa ikiihodhi kwa azimio la upande mmoja.
Rais Abbas amesema
kuwa, “Jerusalemu imekaliwa kimabavu na hatua zote za Israeli ni batili kama
ilivyo katika ujenzi wake wa makazi ya walowezi Jerusalemu ya Mashariki na
maeneo mengine ya Palestina. Ieleweke wazi kuwa,ubadilishaji wa historia ya
Jerusalemu na kuuchafua Msikiti wa Aqswa ni kuchezea hatari,pia ni kushambulia
majukumu ya Palestina na yale ya Jordan.Tunaitahadharisha hilo, isijaribu kusababisha
vita vya kidini wakati mgogoro wetu ni wa kisiasa”.
"Chaguo letu
kama Waarabu na chaguo la dunia ni sheria za kimataifa, uhalali wa kimataifa na
uwepo wa dola huru ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya 1967.Tutatoa
ushirikiano wote katika kufanikisha hilo la kihistoria,ili tupate kuishi kwa
amani pamoja na Israeli. Lakini kama ufumbuzi wa dola mbili utaharibiwa na
kuimarisha dola moja yenye serikali mbili,hapatakuwa na linguine kwetu wala
kwenu ila mapambano na kutaka kupata haki zetu kamili ndani ya Palestina ya
kihistoria. Hivi si vitisho ila ni kutaka haki zetu kama wapalestina”.
Tatizo letu kwa utawala wa kivamizi
wa Israeli sio Uyahudi kama dini, kwani hiyo ni dini ya Mungu kama Uislamu na
Ukristo.Tumebeba majukumu yetu katika Ukanda wa Gaza,ambayo haiwezekani kuwepo
Palestina bila hiyo,ninafarijika leo kuona kufikiwa kwa makubaliano mjini Cairo
kufuatia juhudi nzuri za Misri.Yamekomesha vitendo vya Hamas vilivyoleta
mgawanyiko na hatimae kufanyika kwa uchaguzi mkuu,hatimae serikali yetu mwisho
wa wiki ijayo itakwenda Ukanda wa Gaza ili kufanya kazi huko.
"Ukimya wa jumuiya ya kimataifa
juu ya vitendo dhalimu vya Israeli,ndio uliohamasisha vitendo hivyo tangu awali
hadi inakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake, uko wapi Umoja
huo na maazimio yake?Vipi unatendea mataifa kwa viwango tofauti? Basi huu ni
wajibu wa Umoja wa Mataifa." Aidha ameuomba kumaliza uvamizi wa Israeli ndani
ya muda maalumu,kwani haiwezi tena kutoa data huru kuhusu mpango wa amani wa
kiarabu,hasa kuhusiana na faili wakimbizi kwa mujibu wa azimio la Umoja wa
Mataifa 194,huku akiashiria kuwa maazimio ya Umoja wa Mataifa yanaendelea
kupuuzwa na Israeli”.
Rais Abbas amesisitiza haja ya
kusitisha shughuli za ujenzi wa makazi ya walowezi katika maeneo ya Palestina,kwani
hatuna uwezo wa kulinda raia zetu chini ya utawala wa mabavu,Umoja wa Mataifa
uitake Israeli kutambua mipaka Palestina ya mwaka 1967 na kupunguza mpaka na
kuomba wajumbe wote wa Umoja wa Mataifa kutangaza kwamba kutambuliwa kwao kwa
msingi wa mipaka ya 1967,pia wanachama wote wa Umoja huo kutambua mipaka hiyo
ili kutilia mkazo maazimio ya sheria za kimataifa.
Amesema:"Iko wapi mipaka ya
Israeli mlioitambua wakati Israeli yenyewe haijaikubali,sheria za kimataifa
zinaitaka dunia kuweka hiyo mipaka". Aidha Rais ametoa wito kwa nchi zote
duniani kutoshiriki katika ujenzi wa makazi ya kikoloni ulio kinyume na
sheria,huku zikichukua hatua stahiki dhidi yake kama ilivyofanya jumuiya ya
kimataifa dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Afrika ya kusini na tunataka
kutangaza habari mbaya za mashirika ambayo yanafanya kinyume cha sheria na
makazi."
Hivyo,amezihimiza nchi wanachama
kuitambua dola ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967,huku akitilia
mkazo kuwa hatua hiyo haitoathiri mpango wa amani,hasa hasa ikiwa Wapalestina
wanaitambua dola ya Israeli. Tunauhimiza Umoja wa Mataifa kuikubali Palestina
kama mwanachama wake kamili,huku tukiiomba jumuiya ya kimataifa kuendelea
kuisaidia kiuchumi na kifedha ili iweze kujitegemea na kujiamini.
Aidha Rais Abbas,ametahadharisha
juhudi za kutaka kubadilisha majukumu ya shirika la misaada UNRWA na kanuni zake,pia kufuta kipengele cha
saba katika Baraza la haki za binaadamu au kuzuia kutoa orodha chafu ya
mashirika yanayofanya kazi katika makazi ya walowezi wa Israeli nchini
Palestina inayokaliwa kimabavu.
Rais Abbas amehitimisha hotuba yake
kwa kutilia mkazo msimamo wa nchi yake,katika kuheshimu haki za binaadamu na
kutekeleza mikataba ya Umoja wa Mataifa na ile yote iliyosaini,kwani Palestina
ni sehemu ya jumuiya ya kimataifa na si vingine. Huku nchi yake pia itaandaa
matakwa hayo kwa maazimio yatayokwenda sambamba na misingi husika,kisha
kuyawasilisha kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
=== ===
===
No comments:
Post a Comment