Habari za Punde

WAAMUZI WA ZANZIBAR WALIOFAULU COOPER TEST HAWA HAPA

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kamati ya Waamuzi Visiwani Zanzibar imetangaza majina ya Waamuzi waliofaulu katika mtihani wa utimamu wa mwili (Kopa Test) uliofanyika juzi Amani Mjini Unguja.

Akizungumza na Mtandao huu katibu wa Kamati ya Waamuzi Zanzibar Muhsin Ali "Kamara" amesema jumla ya Waamuzi 56 walifanya mtihani huo  ambapo Waamuzi 34 ndio waliyofaulu huku Waamuzi 22 walifeli.

Kamara amewataja Waamuzi hao 34 waliofaulu ni Omar Abdallah Khamis, Kassim Suleiman Sereji, Mohammed Khamis Mwadin, Mohammed Ali Mohammed, Nassor Salum Masoud, Ali Ramadhan Rajab (Kibo mdogo), Nassir Salum Sihai (Msomali), Abeid Juma Khamis na Iddi Khamis Mberwa.

Wengine ni Mariam Chalse Mattius, Ruwaida Abdallah Khamis, Mwanahija Foum Makame, Dalila Jaffar Mtwana, Mgaza Ali Kinduli, Mbaraka Haule Haule, Mfaume Ali Nassor, Rashid Farahan Issa (Webb), Mohammed Kassim Mohammed, Mohammed Omar Haji, Omar Bakar Omar, Mohammed Rajab Mgeni, Mustafa Abdallah Khamis, Sharifu Haji Mohammed, Issa Haji Vuai, Ramadhan Keis Ramadhan, Ame Abdallah Khamis, Peter Masele Juma, Mussa Hemed Iddi, Omar Khamis Juma, Abdallah Ali Abdallah, Machano Ali Khamis, Mohammed Hassan Nassor, Suleiman Karim Khatib na Suleiman Zaharan Ali. 

Waamuzi hao watasimamia Mashindano yote yanayosimamiwa na ZFA Taifa ikiwemo ligi kuu, daraja la kwanza na la Pili Taifa kwenye msimu mpya wa mwaka 2017-2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.