Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Akifungua Kituo Cha Mkono Kwa Mkono Micheweni Kisiwani Pemba

WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo, (kulia) akikata utepe kuashiria kukifungua Kituo cha Mkono kwa mkono, kilichopo hospitali ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, akiwa na Mratibu Mkuu wa masuala ya ulinzi na uhifadhi wa mtoto, kutoka shirika la Save Children Zanzibar Ramadhan Mohamed Rashid
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo, akitembea kuelekea kwenye mazungumzo na wananchi, wanafunzi na madaktari wa Hospitali ya Micheweni, mara baada ya kukifungua Kituo cha Mkono kwa mkono kilichopo hospitalalini hapo, akiwa na Mratibu Mkuu wa masuala ya ulinzi na uhifadhi wa mtoto, kutoka shirika la Save Children Zanzibar Ramadhan Mohammed Rashidi
WASOMA utenzi kulia ni Suria Said Ali na kushoto Twalhia Hatoro Hamad, wakihanikiza utenzi huo kwenye hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Mkono kwa mkono, kilichopo hospitali ya Micheweni
MSOMA risala Mgeni Haroun Salim, kwenye hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Mkono kwa mkono, kilichopo hospitali ya Micheweni, kazi iliofanywa na waziri wa afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo

WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo, akizungumza na wanafunzi, wazazi na watendaji wa Hospitali ya Micheweni, mara baada ya kufungua kituo cha Mkono kwa mkono kilichomo hospitalini hapo
WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo, akiwaonyesha wananchi wa wilaya ya Micheweni, hati aliokabidhiwa kutoka kwa Mratibu wa Save the Children, mara baada ya kukifungua kituo cha Mkono kwa mkono, kilichopo hospitali ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba

Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba, wakimsikiliza Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akihutubia wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Kituo cKIliohudhuria hafla ya ha Mkono kwa Mkono katika hospitali ya Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba, wakimsikiliza Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akihutubia wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Kituo cKIliohudhuria hafla ya ha Mkono kwa Mkono katika hospitali ya Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Wananchi na madakatari wanaofanyakazi hospitali ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba, waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkono kwa mkono, kilichopo Hospitali ya Micheweni, kazi iliofanywa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo.
(Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.