NA HAJI NASSOR, PEMBA
WENYEJI wa uwanja wa Gombani timu ya Younger Islanders
inayokipiga ligi ya Zanzibar kanda ya Pemba, jana ilidhihirisha kuwa wanapokuwa
ndani ya nyasi bandia, hutembeza kipigo, baada ya jana tena kuichapa Chuo basra
kwa mabao 3-0.
Katika
mchezo wa awali waliocheza kwenye uwanja huo,Oktoba 19, iliiyeyusha Shaba kwa
bao 1-0, ingawa walipotoka nje ya dimba hilo Okotba 13, walipachikwa bao 1-0 na
FSC.
Kwa
jana ndani ya dimba hilo la Gombani, walianza mchezo vyema, huku wapenzi na
washabiki wao wakianza kunadia bao, kunako dakika ya 23, baada ya mpira
ulioamba ambaa kwenye kibendera cha kona, na kumfikia Ali Khamis, aliefunga
bao.
Chuo
basra wajikaza sana baada ya kuingia kwa bao hilo, na kujaribu mashuti ya mbali,
kila walipokuwa wakipata nafasi, lakini yote yalikuwa chakula mbele ya mlinda
mlango wa wenyeji wao.
Dakika
tano kabla ya mapunziko (40), Abubakar Habibu aliipatia Islnders bao la pili,
baada ya uzembe wa mwaka, uliofanywa na walinzi wa Basra, na kisha mfungaji
kuutumia mwanya huo, na kwenda mapunziko wakiwa mbele kwa mabo 2-0.
Kipindi
cha lala salama, Basra walianza kwa mwendo kasi, huku wakifanya mabadiliko ya
wachezaji, ili wajinasue na kipigo hicho, lakini walijikuta wakikatishwa tamaa na
Mohamed Khamis kunako dakika ya 80, kwa kuwapachika bao la tatu.
Katika
uwanja wa FFU Finya, timu isiotabirika ya Okapi iliotokea kwenye nane bora
msimu uliopita, waliwakaanga Hard Rock kwa mzinga 1-0.
Kwa
matokeo hayo sasa, Islanders, Mwenge na FSC ndizo timu zinazokabana koo, kwenye
kiti cha uongozi wa ligi kuu ya Zanzibar kituo cha Pemba, kwa point sita kila
timu, huku timu za Okapi na News star zikiwa na point nne nne, ingawa hadi sasa
timu ambayo haijavuna pointi, ni Wawi star ambayo ishashuka dimbani mara mbili.
Leo
kutakuwa na mchezo mmoja tu wa ligi kuu ya Zanzibar kituo cha Pemba, kwa Shaba
yenye polint tatu, itaumana na New star yenyewe ikiwa na point nne, ambapo
kesho ni zamu ya Opec yenye point moja, watakaovutana na Kizimbani yenye point
tatu, kwenye uwanja wa FFU Finya.
No comments:
Post a Comment