Habari za Punde

LIGI KUU ZENJ KUINGIA MZIGONI TENA KESHO MIEMBENI CITY KUKIPIGA NA CHUONI

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Mzunguko wa nne wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja utaanza kesho kwa kupigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Amaan kati ya Chuoni dhidi ya Miembeni City majira ya saa 10:00 za jioni.

Chuoni inakwenda katika mchezo huo wakiwa na alama 4 wakishika nafasi ya 6 huku Miembeni City wenyewe wakijitupa katika mchezo huo wakiwa na rekodi mbaya yakupoteza michezo mitatu mfululizo ya awali na wakikamata nafasi ya 13 katika timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.