Habari za Punde

Mtanzania Aibuka Mshindi Mbio za KMKM 10 KM Marathon Zanzibar leo.

Mtanzania Dikson Marwa kutoka Musoma aibuka mshindi wa Mbio za KMKM 10 KM Marathon kwa kukimbia kwa muda wa dakika 29;52.02, Mbio hizo zimeazia katika viwanja vya Kambi ya KMKM kibweni na kumalizia katika viwanja vya Mpira maisara Zanzibar, 

Mshindi wa Pili katika Mbio hizo 10 KM alikuwa mkombiaji kutoka Nchini Kenya aliyekimbia kwa dakika 29:52.07 Lamek Mwakiya na mshindi wa Tatu katika mbio hizo kwa upande wa wanaume alikuwa Nelsonpry Mbuyu aliyekimbia kwa dakika 29:59.02 kutoka JKU Zanzibar.

Na kwa upande wa Wanawake katika Mbio hizo za KMKM 10 KM Marathon alikuwa mkimbiaji kutoka Sara Ramadhani kutoka Arusha Tanzania amekimbia kwa dakika 37;38.25, Nafasi ya Pili imeshikiliwa na mkimbiaji kutoka Kenya Sharon Mruyuti  aliyekimbia kwa muda wa dakika 37;38.43 na nafasi ya Tatu kwa upande wa wanawake imechukuliwa na mkimbiaji kutoka Arusha Tanzania Zakia Mrisho aliyekimbia kwa muda wa dakika 38:43.48. Mbio hizo zimeandaliwa na Jeshi la Kuzuiya Magendo Zanzibar (KMKM) 

 Hii ikiwa ni mara ya Tatu kuandaa mbi hizo za KMKM 10 KM na kushirikisha wakimbiaji kutoka sehemu mbalimbali na kutambuliwa Kimataifa.
Washiri wa Mbio za KMKM 10KM zikiaza katika eneo la kibweni Zanzibar na kuelekea katika viwanja vya mpira maisara Zanzibar katika mbio hizo zimewashirikisha wakimbiaji 120 na kwa Upande wa Wazee waliokuwa na umri wa miaka 70 walishiriki 30 wao wameaza kwa 2KM na kumalizia katika viwanja vya maisara walianzia michezani kisonge. 
Washiriki wa Mbio za KMKM 10 KM wakijiandaa kuaza kwa mbio hizo katika eneo la kibweni Zanzibar.
Washiriki wa Mbio za KMKM 10 KM wakijiandaa kuaza kwa mbio hizo katika eneo la kibweni Zanzibar.
Kundi la kwanza la wakimbiaji wa mbio za KMKM 1O KM Marathon wakikatika katika mitaa ya mtoni wakielekea  katika kituo cha kumalizia mbio hizo viwanja vya maisara kundi hili ndilo lililotowa mshindi wa Kwanza, Pili na wa Tatu wa mbio hizo.
Kundi la kwanza la wakimbiaji wa mbio za KMKM 1O KM Marathon wakikatika katika mitaa ya kinazini wakielekea  katika kituo cha kumalizia mbio hizo viwanja vya maisara kundi hili ndilo lililotowa mshindi wa Kwanza, Pili na wa Tatu wa mbio hizo.
Washiriki wa mbio hizo kutoka Upendo Lottle Bredholt aliyeshika nafasi ya 43 kwa upande wa wanawake na Nik Bredholt ameshika nafasi ya 138 kwa upande wa Wanauma wakimbaliza mbio hizo katika kituo cha kumalizia katika viwanja vya maisara Zanzibar ni wageni peke kutoka Nje ya Afrika walioshiriki mbio hizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.