Habari za Punde

Timu ya Jangombe Boys Yahenyeshwa na Black Sailors.

Wachezaji wa Timu ya Black Sailors wakishangilia bao lao la ushindi dhidi ya Timu ya Jangombe Boys lililofungwa na mshambuliaji wake Abass Peter. katika dakika ya 75 ya mchezo kipindi cha pili.(Picha na Othman Maulid)
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mzunguko wa pili wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja umemalizika jioni ya leo ambapo timu ya Black Sailors (Mabaharia Weusi) wameichapa Jang’ombe Boys bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Amaan.
Bao pekee la Sailors lililopeleka furaha kwa kocha wao Juma Awadh limefungwa na Abbas Peter John dakika ya 75 ya mchezo huo.
Mzunguko wa tatu wa ligi hiyo utaanza Jumamosi ya Oktoba 21 saa 8:00 za mchana katika uwanja wa Amaan kati ya Mafunzo na Taifa ya Jang’ombe na saa 10:00 za jioni kati ya JKU na Miembeni City.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.