Habari za Punde

Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Yaangamiza Tani 11.6 za Maziwa na Bidhaa Mchanganyiko Zilizoharibika Kwa Kumaliza Muda wa Matumizi Yake.

Meneja wa Kampuni ya Farid Supply iliyoingiza maziwa hayo Mansour Said akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu ya sehemu ya maziwa hayo kuharibika.
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakishusha maziwa tani 11.6 na bidhaa mchanganyiko zilizo haribika kwa ajili ya kuangamizwa katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
Kijiko likiangamizwa maziwa yaliyoharibika pamoja na bidhaa mchanganyiko katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Idara ya Udhibiti na Usalama wa chakula Dkt. Khamis Ali Omar (wambele) akisimamia ungamizwaji wa bidha zilizoharibika katika dampo la Kibele.

Na Ramadhani Ali – Maelezo    18.11.2017                                       
Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini kutoka nje wameshauriwa kutoogopa  gharama wakati wa kusafirisha bidhaa zao na wahakikishe wanatumia njia bora za usafirisha ili mizigo yao ifike ikiwa salama.

Mkuu wa Idara ya Udhibiti na usalama wa chakula wa Bodi ya Chakula na Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Khamis Ali Omar ametoa ushauri huo wakati wa  kuangamiza tani 11.6  za maziwa katika dampo la Kibele yaliyoingizwa nchini baadhi yakiwa yameharibika kutokana na usafirishaji mbaya.

Alieleza kuwa sehemu ya maboksi ya maziwa yalipasuka na kuharibu mengine na baada ya kuyafanyia uchunguzi walijiridhisha kuwa yalikuwa hayafai kwa matumizi ya binaadamu.

Alisema waliishauri Kampuni iliyoiingiza maziwa hayo Farid Supply kuyarejesha yanakotoka ama kuyaangamiza baada ya kuona yako katika hali hatarishi ya afya za wananchi na walikubali yaangamizwe ili kupunguza gharama ya kuyarejesha.

Dkt. Khamis aliwataka wafanyabiashara kuelewa kuwa kunatafauti kubwa ya kusafirisha vyakula vya maji maji na bidhaa nyengine za kawaidi na vyakula vya maji maji vinahitaji tahadhari kubwa zaidi wakati wa kusafirishwa.

Alisema lilijitokeza katika kusafirisha maziwa hayo ni kukosekana umakini na  kusababisha kontena lililobeba maziwa kuserereka wakati wa safari na baadhi ya maboksi yalianguka na kuapasuka nadani ya kontena hilo.

Meneja wa Kampuni ya Farid Supply Mansour Said ambae alishiriki katika zoezi hilo Kibele, alikubali kuwa kulitokea tatizo katika kontena hilo na baadhi ya maboksi ya maziwa yalipasuka lakini sehemu kubwa ya maziwa hayo yalikuwa hayajaharibika na yalikuwa yanafaa kutumika.

Alisema maziwa hayo yaliyokuwa na thamani ya zaidi ya sh. 52 milioni huenda yalianza kuharibika baada ya kuzuiliwa kwa kwa kipindi cha miezi nane katika bandari ya Zanzibar .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.