Habari za Punde

Hatimae Timu ya Taifa ya Jangombe Yafanikiwa Kupata Ushindi wa Kwanza Ligi Kuu ya Zanzibar Kwa Kuifunga Timu ya Miembeni City, Wao Dakika 450 Hawana Goli Hata Moja.Timu ya Taifa ya Jang'ombe (Wakombozi wa Ngambo) leo kwa mara ya kwanza wamefanikiwa kupata ushindi katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja baada ya kuichapa Miembeni City mabao 2-0 katika mmchezo uliopigwa saa 10 za jioni kwenye uwanja wa Amaan.

Mabao ya Taifa yamefungwa na Muharami Salum (Marcelo) dakika ya 55 na Abdul Azizi Makame (Abui) dakika ya 90.

Kwa matokeo hayo Taifa wamefikisha alama 6 katika michezo mitano waliyocheza baada ya kufungwa mmoja sare mitatu na kushinda mmoja wakati Miembeni city wameendelea kuweka rikodi mbaya baada ya kufikisha dakika 450 kwa michezo mitano pasipo kufunga bao hata moja kwenye ligi hiyo wakiwa wana alama moja pekee kufuatia kufungwa michezo 4 na sare mmoja.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika Uwanja wa Amaan ambapo saa 8:00 za mchana Jang'ombe Boys watacheza na Charawe na saa 10:00 za jioni Black Sailors watakipiga na Zimamoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.