Habari za Punde

Mchezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar Mohammed Mmanga Anyakuwa Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi.

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
BEKI kisiki anayekipiga ndani ya klabu ya Polisi, Mohammed Othman Mmanga amechaguliwa kuwa mchezaji bora ndani ya klabu hiyo katika mwezi Oktoba, 2017 kutokana msaada mkubwa alioutoa ndani ya kikosi hicho katika michezo iliyopita ya ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja.

Mmanga ambaye ndio mchezaji pekee kutoka klabu hiyo kuitwa katika timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Hereos), amekuwa na msaada mkubwa katika idara ya ulinzi, na kusababisha timu hiyo kuruhusu mabao 3 katika michezo 6 ya ligi waliocheza. 

Utaratibu wa kutoa zawadi ya mchezaji bora ndani ya klabu ndio kwanza umeanzishwa kwa mwezi Oktoba na utatolewa kila mwezi, kwa lengo la kuwapa motisha wachezaji ili waweze kujituma zaidi na kuwapa zawadi ya Kikombe pamoja na cheti.

Kwenye msimamo Polisi wapo nafasi ya 7 wakiwa na alama 8 kwa michezo 6 waliocheza ndani ya ligi hiyo yenye jumla ya timu 14.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.