Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Atoa Msaada Kwa Msikiti wa Noor Kijji Cha Mkange Miono Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo.

Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy akimkabidhi Imamu wa Msikiti wa Noor kijijini Mkange, Miono, Wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani Sheikh Khamis Nassor wakati alipowasilisha msaada wa zulia la kuswalia msikitini hapo akiwa kaongozana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Jaffary Haniu (nyuma ya Imamu) leo Novemba 17, 2017

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of ArmsKURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waumini wa dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo katika Kijiji cha Mkange, Miono,  Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani ,wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada wa zulia la kuswalia na fedha taslim Shilingi milioni Mbili.
Zulia pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti huo Alhaji Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani.
Mara baada ya kukabidhi Zulia na fedha hizo, Kanal Mkeremy kwa niaba ya Rais Magufuli amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo lililokusudiwa.
Akiungumza mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo, Sheikh Nassor amesema kwa niaba ya waumini wa Msikiti huo wanamshukuru Mhe. Rais kwa kuitikia ombil lao la kupata zulia, na kwamba  kwa kutimiza ahadi yake hiyo Mhe. Rais amedhihirisha kuwa yeye ni mtu wa watu asiyebagua dini wala kabila katika kusaidia jamii ya kitanzania.
Sheikh Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea  kumuombea Mheshimiwa Rais na kuwataka watanzania wote nchinikuungana nao kumuombea Rais bila kujali itikadi za kisiasa ama imani za kidini kwani anayoyafanya Rais kwa wananchi wa Tanzania ni kwa manufaa ya wananchi wote.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Pwani

17 Novemba 2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.